Majadiliano:Orodha ya wanawake shujaa

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lemma??[hariri chanzo]

Sielewi lemma hiyo. Ni tafsiri ya en:List of women warriors in folklore (bila kuiunganisha na makala ile). en:Warrior si sawa na shujaa. Shujaa ni neno pana zaidi, mara nyingi haina uhusiano na vita. Pamoja na hayo, makala ya enwiki machoni pangu si makala inayofaa kutafsiriwa neno-kwa-neno kwa Kiswahili. (sielewi sehemu ya kwanza ya makala kwa Kiswahili). Tena ni dhahiri makala ya enwiki ni dalili ya majadiliano kwenye utamaduni ya Marekani. Sielewi jinsi gani miungu ya dini za kale zinafaa kuitwa "warrior" hata kama ni miungu ya vita? Pamoja na kuorodhesha wanawake waliokuwa wahalifu, majambazi, wahanga wa nyakati zao. Tena makala ya enwiki inabana mifano yake katika orodha kwa hao walioingia katika fasihi na mapokeo ya kiutamaduni (folklore) . Sijui tufanye nini? Kipala (majadiliano) 11:31, 31 Machi 2021 (UTC)[jibu]