Majadiliano:Nadir Haroub Ali

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Masahihiho ya lazima[hariri chanzo]

Silausi salaam, unahitaji kusafisha kasoro kadhaa, hasa tahajia na kutunga sentensi sanifu. (Naomba wenzangu tumwachie kazi hii tuone kama anaweza mwenyewe!)

  • lemma: "Nadir haroub Ali" iwe "Nadir Haroub Ali" - tumia menyu ya "more" + "hamisha" - kwenye dirisha la "Kuelekeza jina jipya:" uandike Nadir Haroub Ali, baadaye thebitisha
  • Maneno ya kwanza yaani Lemma=jina la mwenyewe kwenye makala yawe kwa maandishi koze. Nimewahi kukumbusha kuhusu hiyo, ni utaratibu hapa.
  • Hakuna jamii kwa makala ambayo ni kosa sana (ambalo mimi nimelifanya pia wakati wa kuchoka, hata hivyo kosa zito!).
  • Sentensi ya kwanza imemaliza baada ya "Yanga Sc". Hapa unapaswa kuweka nukta na kuanza sentensi ya pili (herufi kubwa kwa neno ya kwanza).
  • hakuna sababu kuandika "Beki", "Nahodha" na "Taifa" kwa herufi kubwa si neno la kwanza katika sentensi wala jina. Ziwe kwa herufi ndogo.
  • Hajazaliwa "Februali" bali "Februari" (hata tukijua sote kuna vita ya r/l kwenye mkoa wa Mbeya, wikipedia hii inasaidia kushinda!)
  • Kiswahili cha "timu hio" ni "timu hiyo"
  • Siyo katikati ya maneno " mwaka 2016 Machi" ni sentensi moja inayokwisha na nyingine inayoanza?? Basi: nukta iwepo
  • Canada kwa Kiswahili ni "Kanada", Vancover kwa lugha yote ni "Vancouver"
  • "Kuhusu Kucheza" iwe "Kuhusu kucheza"
  • Halafu inafaa kujaribu mabano mraba [[ ]] pale ambako nchi au mahali hutajwa, maana labda kuna tayari makala ya wikipedia. Ukibofya "Onyesha hakikisho la mabadiliko" utaona kama neno litakuwa buluu (=makala ipo, mabano yabaki) au nyekundu (hakuna makala bado, si lazima kuweka mabano). Jaribu hii kwa kila mahali kuanzia mahali pa kuzaliwa hadi "Vancouver".

Wasalaam --Kipala (majadiliano) 19:53, 22 Aprili 2016 (UTC)[jibu]