Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Muhammad Ahmad ibn Abd Allah Al-Mahdi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mohammed Ahmad ibn Abd Allah (*12 Agosti 1844 22 Juni ) alikuwa mwenyeji wa Sudani aliyejitangaza kuwa ndiye mahdi. Alifaulu kuunganisha makabila mbalimbali ya nchi kwa vi1885ta ya jihadi akamaliza utawala wa kikoloni wa Misri iliyosaidiwa na Uingereza na kuanzisha Dola la Mahdi.

Baada ya miaka ya kufundisha Uislamu na kusafiri nchini Sudani Muhammad Ahmad alijitangaza kuwa al-Mahdi al-Muntazar (mwokozi anayetarajiwa) mwaka 1881. Katika barua ya tarehe. 29 Juni 1881 aliwaeleza Wamisri ya kwamba aliteuliwa kuunganisha nchi zote za Waislamu na kurudisha uataratibu wa siku za Mtume Muhamad.(S.A.W)

Gavana Mmisri alijaribu kumkamata lakini askari zake walishambuliwa na kuuawa na wafuasi wa al-Mahdi. Baada ya haya Muhamad Ahmad alitangaza vita ya jihadi akafaulu kukusanya maansar au wasaidizi wengi. Watu walimfuata kwa sababu mbalimbali. Wengine hasa watu wengi maskini walimwamini ndiye al-Mahdi wa Allah. Viongozi wa makabila ya Waarabu walichukia utawala wa Wamisri wakamkubali kama kiongozi atakayewaondoa. Wengine walikuwa walikuwa wakitajirika kwa njia ya biashara wa watumwa wakakasirika majaribio ya serikali ya Misri iliyotaka kukandamiza biashara hii.

Katika mapigano mablimbali maasar waliweza kushinda hjeshi za Wamisri na kukamata bunduki nyingi pamoja na risasi na dhahabu. Kilele cha jiahdi ilikuwa kutekwa kwa mji mkuu wa Khartum tar. 26 Januari 1885. Gavana Mkuu jenerali Gordon Pasha aliuawa. Al-Mahdi alianzisha mji mkuu mpya Omdurman kando la mto Nile ng'ambo ya Khartum uliokuwa mji mkuu wa Dola la Mahdi.

Hapa aliaga dunia tarehe 22 Juni 1885. Dola lililoanzishwa naye likaendelea hadi 1895 likavamiwa na jeshi la Waingereza pamoja na Wamisri na kurudi chini ya utawala wa nchi hizo.

Start a discussion about Muhammad Ahmad ibn Abd Allah Al-Mahdi

Start a discussion