Majadiliano:Mtume Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jina na nafasi kati ya mitume[hariri chanzo]

  1. Si wazi ya kwamba jina la kuzaliwa lilikuwa "Shimon bar Yona"; chanzo chake ni Mt 16,17 ambako Yesu anamwita "bar yona" (maneno mawili= mwana wa Yona); lakini katika Yoh 1,42 anamwita "mwana wa Yohane". Kuna wataalamu wanaojaribu kuunganisha habari hizi mbili kama maumbo mawili la jina lilelile kwa Kiaramu na Kigiriki; ila tu kuna wengine waisokubali kwa sababu kuna pia neno la "baryona" (neno moja) lenye maana ya "mwenye hasira" na hii imechukuliwa kama daili ya kwamba hata Petro alitokea kati ya magaidi Wayahudi waliopambana na Waroma.
  2. Si wazi ya kwamba Petro alikuwa wa kwanza kati ya mitume wala kuwa askofu wa kwanza wa Roma. Hii ni mafundisho ya kanisa katoliki na inafaa kuelezwa hivyo. Kuna sababu nzuri kuamini hivyo lakini kuna pia sababu nzuri ya kupinga hoja hizi. --Kipala (majadiliano) 11:34, 21 Septemba 2008 (UTC)

Kuhusu jina "Bar-Yona" si jambo muhimu, lakini rai ya kuwa Simoni alikuwa gaidi kwangu ni ngeni. Bila ya shaka wanaosema hivyo si wengi. Kuhusu yeye kuwa "wa kwanza" imeandikwa wazi katika Injili (kwa Kigiriki "protos"), ndiyo maana anashika nafasi hiyo katika orodha zote nne za Agano Jipya. Kwamba alikuwa "askofu" wa Roma, mimi pia sikubali, kwa sababu askofu ni mwandamizi wa mitume, kumbe mtume ni wa pekee. Hata hivyo niliandika kuwa "Wakristo wengi" (si wote) wanamuona kuwa "papa" wa Roma kwa maana ya kuwa maaskofu wa mji huo (wanaoitwa hivyo) ni waandamizi wake katika kuongoza Kanisa hilo. --196.45.46.171 09:28, 24 Septemba 2008 (UTC)

Umbo la jina bar-yona au baryona pamoja na tendo la Petro kushika silaha wakati wa kukamatwa kwa Yesu imesababisha wataalamu kadhaa kuuliza kama alikuwa Kiasili Zelote kame Simoni mwingine na labda pia Yudas. Lakini kweli si muhimu sana ni maswali-maswali tu.
Petro na Roma ni jambo pana. Kuna wataalamu wengi ambao hawakubali ya kwamba Petro alifika Roma; mapokeo ya kuwa Petro aliongoza kanisa huko Roma pia kufa huko hayana uhakika kihistoria.
Kuna maelewano ya kwamba Petro alikuwa kati ya viongozi wa kanisa la kwanza lakini Biblia inaonyesha viongozi mbalimbali. Hakuna uthebitisho ya kwamba Petro alikuwa kiongozi mkuu;
Kwa jumla mafundisho kuhusu Petro ni tofauti kati ya kanisa Katoliki na makanisa mengine kama Waorthodoksi au Waprotestant. Hii ieleweke wazi katika makala na lugha yake. --78.51.156.50 21:47, 24 Septemba 2008 (UTC)

Ni kweli kwamba wafuasi wa madhehebu mbalimbali wanakusha kuwa Petro alifika na kufia Roma, lakini msimamo huo unatokana na mabishano ya karne zilizopita dhidi ya Ukatoliki. Hakuna mahali pengine popote duniani panapodai au panapotajwa kuwa Petro alifia huko, tofauti na mitume wengine waliotajiwa miji mbalimbali. Kaburi la Petro linaheshimiwa palepale tangu karne za kwanza. Ushuhuda wa mababu kuanzia Klementi (miaka 30 baadaye) ni mkubwa mno uweze kupingwa. Kuhusu Waorthodoksi wanakubali kabisa ukweli huo; tofauti kati yao na Wakatoliki ni kuhusu yatokanayo nao upande wa Papa. Lakini hata hiyo inazidi kupungua. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:21, 25 Septemba 2008 (UTC)

Kihistoria sikubali. Hakuna kaburi hata moja la mtume yeyote ambalo linaweza kuthebistishwa kihistoria. Naomba nisaidie. Kuna nini kwa Klementi kuhusu kaburi la Petro? Menginevyo tusibishane. Tutafute njia ya kuonyesha hali halisi yaani kuna upana wa mawazo juu ya Petro. Sawa? --78.53.25.203 22:24, 25 Septemba 2008 (UTC)