Majadiliano:Mkunga (samaki)

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

KKK inasema wingi unatumia wa-. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:48, 16 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]

Asante, lakini TUKI inaweka wa- kwa mkunga (midwife) na mi- kwa mkunga (eel). Nadhani hii ni sahihi. Na wewe? ChriKo (majadiliano) 10:13, 16 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]
Vivyo hivyo tayari Sacleux anatofautisha Mkunga (Sagefemme, accoucheuse) na Mkunga mi- (Anguille, congre, murène). Niko safarini siwezi kuangalia KKK lakini naona mikunga ni sahihi. Vilevile ukiweka "penye mikunga" katika dirisha la google unaona mifano mingi ya mikunga kwa uwingi wa samaki hii. Kipala (majadiliano) 10:28, 16 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]
Hakuna shida. Kamusi zinatofautiana. KK21 inasema pia wa-. Lakini nyingine zina mi- ambayo inafaa zaidi kwa miti ya mkunga. Tuache tu. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:26, 17 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]