Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mkate

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

mkate na dini

[hariri chanzo]

Niliondoa sentensi hii: "Lakini tafsiri hiyo haikuzingatia maneno ya Yesu yanayofafanua aina ya mkate aliyomaanisha: τον επιουσιον, yaani "ulio wa juu kuliko dutu". Naona elezo kitaalamu halilingani na lugha ya Kigiriki. Neno "ἐπιούσιον" (epiousion) si neno linalotokea mara nyingi na hapa wataalamu walihangaika kidogo hata hivyo sioni maana "juu kuliko dutu". Kwa jumla kuna njia mbili kuelewa neno hili [1]:

  • Kutoka ἐπί τὴν oὔsan ἡμέran (epi tēn ousan hēmeran): kwa siku hiyohiyo
  • kutoka ἡ ἐπιούσα ἡμέra (hē epiousa hēmera): siku inayofuata

Ilhali neno ἐπιοῡσα linatokea mara kadhaa katika Agano Jipya kwa maana "siku inayofuata" (yaani kesho) lwa mfano Mdo 7.26 na Mdo 16.11 basi wataalamu wengi wanaelekea kuona ni ombi kwa mkate wa siku inayofuata. Sijakuta maelezo ya kitaalamu yanayodai eti neno linahusu kitu kingine kuliko mkate mwenyewe. Maelezo ya Kiroho ni mazuri kwa maana yao ila tu labda mahali pake si sana katika makala kuhusu "mkate". Kati ya Wakristo inawezekana kuelewa maneno ya Yesu katika Injili ya Luka kwa maana ya Injili ya Yohana (Yn 6,35: εἰμι ὁ ἄρτος τῆς ζωῆς Ndimi mkate wa uhai) lakini katika kamusi elezo iliyo uwanja kwa watu wote mbinu huu uelezwe wazi pamoja na ukosoaji wake.Kipala (majadiliano) 05:05, 7 Julai 2017 (UTC)[jibu]

  1. Vaterunser, 1.2.1. Das Wort ἐπιούσιον katika tovuti ya Bibelwissenschaft.de