Majadiliano:Misingi ya Dini/Usul-din

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Baada ya kuhariri kiasi nimetambua makala ni tafsiri ya sentensi kwa sentensi kutoka https://en.wikishia.net/view/Usul_al-Din. Sina uhakika kama hii inaruhusiwa tukizingatia kanuni za Wikipedia:Hakimiliki. Pamoja na hayo si nzuri tukichukua moja kwa moja lugha ya kidhehebu katika makala za kidini. Nilipoanza kuhriri niliona tayari kwamba makala hii ilisema mara kwa ma "Uislamu" ambako ni lazima kusema "Shia", kwa sababu mambo haiwezekani kudai vile kwa Waislamu wote, na kwa jumla Washia ni idadi ndogo zaidi duniani na Afrika ya MAshariki. Vilevile nilishangaa kidogo kuona walimu (maayatollah) wa dini ambao wanatajwa tu bila kuwaeleza (kama wote wangewajua), kumbe asili ni tovuti ya Kishia.

Nataka kumpa mchangiaji "Pole". Ningependekeza atumie makala za en-wikipedia (zko nyingi) ambako yuko hurui kupanusha sehemu juu ya mafundisho ya Kishia. Ila tu hata kama Mkatoliki anachangia kuhusu mafundudisho ya kikatroliki, si sawa kutumia lugha inayodokeza mafundisho hayo ni "ya kikristo" kama madhebeu mengi yanatofautiana; ni sawa kabisa kuionyesha kama mafundisho ya kikatoliki. Hivyo ndivyo jinsi tunavyotakiwa kuandika kuhusu dini nyingine pia, hapa tukiweza kutambua tofauti zilizopo. Naomba majadiliano hapa na kwenye ukurasa wa ufutaji. Kipala (majadiliano) 18:47, 23 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Mimi nimejitahidi kuhariri michango mbalimbali ya ndugu huyo, nisitambue kwamba alitumia chanzo cha kimadhehebu kisichotakiwa. Hata hivyo, kurasa nyingine zinaeleza tu mambo ya Kishia bila kupinga Wasunni. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:04, 25 Desemba 2021 (UTC)[jibu]