Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mashahidi wa Yehova

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kabla sijaongeza kitu katika ukurasa huu naomba wahusika wasahihishe jina la Yehova katika kichwa kwa kuweka herufi kubwa. Asante. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:23, 26 Julai 2011 (UTC)[jibu]

Riccardo, hakuna wahusika katika Wikipedia. Kila mtu ni muhusika, ilimradi tu, awe anachangia - na wewe n mchangiaji! Una haki zote za kuboresha makala zilizopo. Makala hii haina viwango vya kikiwiki - kwa vile wewe mkali katika hilo. Tafadhali, sahihisha na uongeze nyama!--MwanaharakatiLonga 16:35, 26 Julai 2011 (UTC)[jibu]
Samahani. Naona kama kianzio sio vile.. Kwani Hao mashahidi ni dini au dhehebu tu kama Roma, Anglikana, KKKT na kadhalika? Naona wamepembuliwa kwa mtindo wa kipekee, yaani, kama vile sio sehemu ya waumini wa Ukristo. Nieleweshwe kidogo..--154.73.170.162 13:23, 20 Januari 2016 (UTC)[jibu]
Ni kweli, wanaunda kundi la pekee. Wanajiona hivyo na wanatazamwa hivyo na Wakristo. Makala hii inasema wazi kwamba wengi hawawakubali kuwa Wakristo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:44, 20 Januari 2016 (UTC)[jibu]
Kwa maana hiyo hawafungamani na madhehebu mengine, sahihi? Je, Yesu, si bwana kwao? Nashindwa kuelewa kabisa haoa..--MwanaharakatiLonga 09:52, 23 Januari 2016 (UTC)[jibu]
Ndugu Muddy, dini ya hao ni ya pekee sana. Imetokana na Ukristo, lakini imekanusha mafundisho makuu mengi ya Ukristo. Ndiyo sababu haifungamani na madhehebu yoyote. Watu wote wasio wa kwao ni walaanifu na wataangamizwa milele. Kwa Kiingereza wanajumlishwa katika kundi la "marginal Christians". --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:41, 23 Januari 2016 (UTC)[jibu]