Majadiliano:Kulungu pembe-nne

  Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

  Palahala pembe-nne[hariri chanzo]

  Jambo Rberetta. Umepata jina hili wapi? Ni jina la ajabu, kwa sababu mnyama huyu hafanani na palahala wa kawaida. ChriKo (majadiliano) 21:19, 5 Desemba 2014 (UTC)Reply[jibu]

  ChriKo salaam. Nilipata jina hili kwa kutafsiri jina la Kiingereza "Four-horned Antelope". Mnyama huyu siye mnyama wa Afrika, kwa hiyo nafikiri hakuna jina la Kiswahili litakalotambuliwa. Nilifikiri "palahala" ilikuwa tafsiri nzuri ya familia pana ya "antelope", lakini palahala si ya nusufamilia Bovinae. Jina la Kiingereza pia ni jina la ajabu kwa sababu sawa - "Four-horned antelope" ni "antelope" pekee katika Bovinae.
  Ukipendekeza jina tofauti, tafadhali niambie. Mimi sijui jina lolote katika nusufamilia Bovinae ambalo ni jina pana linalojumlisha spishi kadhaa kama "antelope". Paa au Swala ni majina mapana, lakini siyo ya Bovinae pia. Rberetta (majadiliano) 22:48, 6 Desemba 2014 (UTC)Reply[jibu]
  Nilitafuta tena kwa google, na niliona makala haya: http://sw.swewe.net/word_show.htm/?123594_1&Pembe_swala. Makala hayo yanasema "swala pembe", "pembe swala", "swala pembe-nne", na majina mengine. Lakini siyo makala mazuri - nafikiri yalitafsiriwa kwa kompyuta. Rberetta (majadiliano) 22:48, 6 Desemba 2014 (UTC)Reply[jibu]
  Bila shaka ninafahamu shida yako. Kwa sababu ya hiyo sipendi kuandika makala kuhusu wanyama wasiotokea Afrika. Lakini ukijaribu kufanya hii, tumia jina la kienyeji (kama Saola) au tafuta jina la Kiswahili la mnyama aliye na mnasaba na somo lako au anayefanana na huyu. Sasa, ufafanuzi wa "antelope" ni mnyama wo wote katika Bovidae ambaye siyo ng'ombe, nyati, baisani, mbuzi au kondoo. Kwa hivyo, "swala" lingefaa. Lakini ukisema kwamba "swala" ni kwa wanyama wanaofanana na "gazelle", kuna "antelopes" katika Bovinae pia. Ningependa "kulungu" kwa sababu mnyama huyu ni mdogo kiasi kama "four-horned antelope". Kila la heri! ChriKo (majadiliano) 00:09, 7 Desemba 2014 (UTC)Reply[jibu]
  Je, unapendekeza "Kulungu pembe-nne"? Ningependa hilo. Sikuzingatia jina hilo kwani mimi sikuwa na hisia kwamba jina kulungu lilikuwa jina la kundi la wanyama, kama swala. Jina kulungu ni la nusufamilia Bovinae, kwa hiyo ninalipenda kuliko palahala. Na kweli "four-horned antelope" anafanana na kulungu kuliko palahala. Ukilipenda "kulungu pembe-nne", nitalibadilisha hivyo. Rberetta (majadiliano) 01:14, 7 Desemba 2014 (UTC)Reply[jibu]
  Ndiyo, "kulungu pembe-nne" ni bora. Badilisha jina tafadhali. ChriKo (majadiliano) 14:46, 7 Desemba 2014 (UTC)Reply[jibu]