Majadiliano:Kichina cha Xiang
Mandhari
Salaam Dokta Stegen.. Tazama hii:
'KI-VI Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilima Chakula kimekwisha
- Vyakula vimekwisha
- Kijito kimekauka
- Vijito vimekauka
- Kijito kimekauka
- Vyakula vimekwisha
Hivyo basi haiwezi kuwa "Kichina "ya" Xiang.. Ni Kichina "cha" Xiang...
- SamahaniLakini
wako, --MwanaharakatiLonga 17:44, 12 Septemba 2016 (UTC)
- Bila samahani, ndugu! Kwa muda mrefu niliandika nilivyofundishwa, kwamba nchi na lugha hazifuati ngeli. Ingawa jina la Uingereza liko katika ngeli ya u- (kama upendo, urafiki n.k.), vitenzi vyake huanza na i-, k.m. katika sentensi "Uingereza yapata pigo baada ya kujitoa kwenye umoja wa ulaya (EU)." Hata hivyo lugha imeanza kubadilika (na kubadilika ni lazima katika eneo la lugha). Siku hizi napata sentensi kama ifuatavyo namba 1 zaidi kuliko namba 2:
- Hivi leo, Kiswahili kimekua na kinazungumzwa na watu zaidi ya milioni 120 duniani.
- Kiswahili imefikia hatua sasa inafundishwa katika vyuo vikubwa duniani.
- Je, nibadilishe sentensi zote zenye "Kilugha i-..." ziwe "Kilugha ki-..."? Niambie tu. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 21:15, 12 Septemba 2016 (UTC)
- We bwana huwezekani. Pamoja na hayo, hata kwa kusikika tu, huwezi kuipenda kwa Kichina "ya" - labda uangalie mifano yako mengine.--MwanaharakatiLonga 16:37, 13 Septemba 2016 (UTC)