Majadiliano:Kiazi
Mandhari
Ni kweli ya kwamba matumizi ya kiazi na tunguu yanalingana na vikundi vya kibiolojia?
Tutapanusha namna gani? Nikiangalia en:Tuber kati ya "stem tubers" (=viazi vya kizungu au mviringo) na "root tubers" kama vile viazi vitamu. Je, hii inaweza kuelezwa kwa matumizi ya maneno jinsi ilivyoanzishwa hapa? Kipala (majadiliano) 10:02, 13 Juni 2014 (UTC)
- Nakubali kwamba ukarasi huu unahitaji kutanuliwa. Labda nitaifanya hivi karibuni. Lakini ninasisitiza kwamba kiazi ni "tuber" na tunguu ni "bulb". Niliandika kwamba kiazi ni sehemu ya mzizi, kwa sababu kwa matini mafupi hii ni rahisi kufahamu. Kwa kiistilahi kiazi cha kizungu ni sehemu ya shina, lakini hii ni aina maalum ya shina linalofanana na mzizi kwa maoni ya watu wengi. Kwa Kiingereza huitwa "stolon" lakini sijui tafsiri ya neno hili. ChriKo (majadiliano) 20:03, 17 Juni 2014 (UTC)