Majadiliano:Kandete
Haya ni Majadiliano kwa ajili ya kuboresha makala ya Kandete. | |||
---|---|---|---|
|
|
Hii ni makala ya Kandete ipo katika eneo la Wikipedia:Mradi wa Tanzania, juhudi za pamoja katika kuboresha maeneo ya Tanzania kwenye Wikipedia. Iwapo utapenda kushiriki, tafadhali tembelea ukurasa wa mradi, ambapo unaweza kujiunga na majadiliano na utazame orodha ya kazi zilizo wazi. |
Je nini hasa asili ya jina la Kandete.....
[hariri chanzo]Kata ya kandete ambayo ni moja kati ya kata muhimu kabisa zilizo katika wilaya ya Rungwe na ianayo patikana katika bonde maarufu la MWAKALELI. sijui wengine wanasemaje kuhusu kata hiyo lakini nimewahi kusikia kuwa chanzo cha jina hilo ni kutokana na aina ya mimea ijulikanayo kama MATETE.
Najaribu kufikiri na kuona viasili vya ukweli wa mwanzo wa jina hilo kutokana na ukweli kwamba, jamii ya mimea hiyo kuwa mingi katika eneo hilo. Watu wa mazingira hukariri maeneo hayo kama maeneo chepechepe, ambayo kwa mji huo hupatikana kwa wingi sana. kuna maeneo kama barabara iendayo Ipelo karibu na machinjio ya ng'ombe, njia iendayo Ipuguso na Ipyela maarufu kama Ilamba. Barabara ya Sekondari ya Mwakaleli eneo la Centre hapo ni eneo lilokuwa maarufu kwa kuogesha mifugo hasa jamii ya ng'ombe.
Kandete ni mji ulio changamka kwa sasa tofauti na zamani japo naona hofu juu ya kupoteza ile historia yake iliyo bebwa na asili kama uwepo wa vivutio vya Vipepeo vingi vinavyo hama kwa makundi hasa majira ya mwisho wa mwaka, Kunguru Wenye namna ya Plastiki kubwa jeupe kwenye pua zao na ndege wakubwa sana ambao kwa Kikosa lugha kusini mwa afrika 'impududu' na wanyakyusa huita 'imbututu'. Pia ile mito mikubwa kama mto Mwatisi, Lufilyo na mmoja unaobeba jina la kata yaani Kandete.
Nawaza je bado bonde la Mwakaleli litatetea historia na vivutio muhimu vya kiasili vilivyopo na vilivyo salia na vilivyo mbioni kupotea kabisa kwani hofu yangu ni kuwa watetezi wa vitu hivyo hawapo au kama wapo basi hawajui kama vinapotea au wamejisahau kuwa wao ndio wanao wajibika. labda dhana ya kusubiri wahisani iliyo jengeka serikalini imeathiri wananchi. Ni hayo tu naomba msaada wenu kuhusu Kandete hata Bonde la Mwakaleli ikibidi. ,,,,,,,,,,,
Ndandala, B.E
KARIBU KANDETE KITUO CHA BIASHARA
[hariri chanzo]Kandete ni mji unaopatikana katika bonde la mwakaleli ndani ya halimashauri mpya ya Busokelo,Kandete ikiwa ni mji uliozungukwa na vijiji kama vile Isange,Mpombo,Ipelo,Luteba,Lugombo na vijiji vingi vinategemea mji huu kwa biashara ndogo na kubwa ambazo watu wengi huzitumia kama chanzo cha kipato.
Biashara kubwa ndani ya mji huu ni biashara za mbao,viazi mviringo,mahindi,maharage na biashara za usafirishaji.Kutokana na hali ya hewa nzuri ndani ya mji huu watu wwengi wamekuwqa na uwezo wa kustawisha mazao mbalimbali katika msimu wote wa mwaka na kuufanya mji na wakazi wake kuwa na uhakika wa chakula mwaka mzima. Ufikapo Kandete utavutiwa na mtaa wa Majengo kwa biashara mbalimbali mchana na usiku kucha karibu kandete.
Wenu ONGOZWA DAVID SANGA
KANDETE MWAKALELI
kandete ni jina lenye asili lililotokana na matete ambayo hustawi zaidi kwenye chemichemi za maji. Matete haya kwa lugha ya kunyakyusa hujulikana kama "NDETE", Inadaiwa kuwa kandete ya leo hapo zamani ilitawaliwa na mimea hiyo, ambapo kwa sasa mimea hiyo ipo baadhi tu ya maeneo. Hivyo basi kutokana na kuwepo kwa wingi wa mimea hiyo ndipo jina la Kandete lilitokea. Kandete ni kata ambayo ipo katika jimbo la mwakaleli, katika halmashauri ya Busokelo
Ufikapo katika kata ya kandete utapokelewa na watu wenye ukalimu, wenye kujali watu wengine wakizungumza lugha yao ya kinyakyusa, na kiswahili. Lakini kutokana na kuongezeka kwa mwingiliano wa watu utakapofika kandete usishangae kuwakuta watu wa makabila kama vile wakinga, wasafwa, wahehe wabena wandali wanyiha nk, hii ni kutokana na shughuli mbalimbali za kijamii kama vile biashara, kilimo elimu nk. Watu wa kandete hujishughulisha sana kilimo cha mazao ya chakula kama vile mahindi, maharage, viazi, magimbi nk. Lakini pia wapo ambao hujishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara kama vile chai na kahawa. Na biashara nyingine ndogondogo.
hali ya hewa ya kandete na mwakaleli kwa ujumla ni nzuri sana ambayo huweza kuwa kivutio cha utalii wa ndani na wanje. Kuna unyevunyevu wakutosha unasababisha kandete na mwakaleli kwa ujumla ionekane ya kijani wakati wote.
eneo hili limezungukwa na milima ambayo hulipamba kwa uzuru eneo husika.hakika kandete ni sehemu nzuri na ya pekee na ni muhimu sana kama chanzo cha kukuza uchumi wa halmashauri mpya ya Busokelo , mkoa wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla.
Haya ni machache tu kuhusiana na kandete. Tutazidi kujadiliana zaidi katika hariri zijazo kwani utafiti unaendelea kufanyika kuhusiana na kandete na jimbo zima la mwakaleli, na pia halmashauri ya Busokelo.. KHASANTENI SANA. Mungu ibariki kandete yetu, mwakaleli yetu, Busokelo yetu, Mbeya yetu na Tanzania yetu.
wenu mwanakandete halisi.. VICTOR .E. LAMECK
- Wapendwa Victor, Ongozwa, Ndandala, asante kwa michango yenu! Nitahamisha habari kwenye makala penyewe maana hapa ni ukurasa wa majadiliano juu ya makala.
- Itakuwa bora kama mnaamua kujiandikisha katika wikipedia hii, karibuni! Halafu kuchangia kikamilifu.
- Halafu katika kuandika kuna sharti mjitahidi kutumia mfumo wa kamusi: yaani kutotaja yale unayoona au waza (tusiandike "Nawaza je bado bonde la Mwakaleli litatetea historia na vivutio muhimu", au: "Tutazidi kujadiliana zaidi katika hariri") maana hii si habari ni maoni. Ndani ya makala tunaepukana na maoni. Pia hatuongei na wasomaji katika makala za kamusi ( Mungu ibariki kandete yetu, , ASANTENI SANA, Ufikapo Kandete utavutiwa na mtaa wa Majengo).
- Ni sawa ukitumia lugha hii katika kurasa za majadiliano lakini haina nafasi kwenye makala yenyewe. Masharti haya ni jambo la kuzoea. Katika mfumo au style ya kamusi hii pia hatutumii HERUFI KUBWA hapa kuna njia nyingine ya kukazia umuhimu kama vile maandishi koze au chaguo la maandishi makubwa kwa vichwa vya ngazi mbalimbali. Maelezo juu ya haya yanapatikana katika Wikipedia:Msaada wa kuanzisha makala na Wikipedia:Mwongozo. Karibuni! Kipala (majadiliano) 09:22, 14 Desemba 2013 (UTC)
Nina swali kuhusu Mwakaleli: Hadi sasa nimejua tu jina la Mwakaleli lakinini miaka mingi sijafika tena. Sasa baada ya kuona michano hapo juu najifunza kuwa Kandete iko katika "Bonde la Mwakaleli". Lakini nikichungulia sioni Mwakaleli kama jina la mahali yaani hakuna kata ya Mwakaleli. Je mwakaleli ni kijiji au nini? Siku hizi jina la Mwakaleli linataja nini hasa? Kipala (majadiliano) 10:42, 14 Desemba 2013 (UTC)