Majadiliano:Gumbo Kiholota
Mandhari
Sipati picha juu ya maelezo yaliyoongezwa katika ukurasa husika. Maelezo hayaja fuata mwelekeo na taratibu za kamusi elezo hii. Na hisi atakuwa mwenyewe katia mkono wake na kufikiri kwamba alivyoandika ni sahihi. Sijui hata namna ya kuweka maelezo yale sawa. Naona sasa bora kufanya fuatilizi juu ya hili, kwani huyu bwana Gumbo najua wapi pa kumpata na akisha kubali kuwa yeye ndiye aliyeongeza maelezo yale basi atatakiwa kufuata taratibu za kamusi elezo. Niko mbioni kumtafuta....--Mwanaharakati (majadiliano) 12:46, 17 Aprili 2008 (UTC)
- Sijui kama huyu Joslin aliyeandika makala ni Gumba mwenyewe? Au ni yeye mwenyewe aliyeweka nyongeza (anwani 196.1.53.30)? Labda ingekuwa njia kama angeweka haya yote kwenye ukurasa wake wa mtumiaji, halafu kutoa yale yanayofaa kwa makala. Yaani kama mtu anapenda kujitangaza hii ni sawa kwenye ukurasa wake wa binafsi siyo kwenye sehemu za makala. Asante kwa kufuatilia. --Kipala (majadiliano) 22:18, 17 Aprili 2008 (UTC)
- Nimeona bora kuifuta yote kwasababu makala imekosa maelezo ya msingi. Haina mwaka wa kuzaliwa wala historia katika maisha. Pia nilijaribu kumfuatilia, lakini sijakutana nae ila ujumbe niliacha na nilipojaribu kwenda kwa mara ya pili kukawa hamna jibu lolote lile linalohusiana na Wikipedia. Inaonekana hakujali juu ya hili, ingawaje nilipata namba yake ya simu na nikajaribu kumtumia ujumbe mfupi juu ya hili, yeye hakujibu lolote! Basi nimeona hamna sababu ya kuwepo na makala isiofanana na maelezo ya kamusi elezo. Nimeifuta!--Mwanaharakati (majadiliano) 15:03, 24 Aprili 2008 (UTC)