Majadiliano:Greenland

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Grinlandi ?[hariri chanzo]

Nimerudisha uhamisho wa makala kwenda "Grinlandi" uliotekelezwa bila majadiliano. Sababu iliyotajwa wakati wa kuhamisha ni "Greenland ni jina la Kiingereza. "Grinlandi" iliandikwa katika Oxford kamusi ya Kiswahili.". Hii inahitaji majadiliano tukikumbuka tofauti zilizopo kati ya orodha ya majina ya nchi kwa kulinganisha BAKITA, TUKI, na Redio Tanzania Dar es Salaam. Majadiliano haya tulifanya hapa miaka 5 iliyopita. Ikitakiwa tufungue tena.

Kuhusu Grinlandi au Greenland au Grinilandi ni wazi ya kwamba ni nchi isiyojadiliwa sana kwa Kiswahili. Matumizi ya watu wengi (kati ya wachache wanaotumia neno) jinsi ninavyotazama ni "Greenland". Umbo hili limekuwa Kiswahili kutokana na matumzi ya wasemaji chake na kwa hiyo kueleweka zaidi. Swali la umbo sanifu si rahisi kujibu katika mfano kama huu kama mawazo ya wataalamu yanatofautiana. Mtindo wa kutumia pijini ni njia mojawapo. Kimsingi hapa tuna uhurukubwa tukikumbuka kutumia vielekezo vema maana jambi muhimi ni ya kwamba mtu anaweza kukuta makala sawa kama anatafuta Greenland, Grinilandi au Grinland. Ila tu tusibadilishe bila majadiliano maana tunahitaji mapatano juu ya umbo la kimsingi kwa maneno yanayokuja pamoja na jina la nchi kama lugha n.k. Kipala (majadiliano) 07:37, 21 Aprili 2011 (UTC)[jibu]