Majadiliano:Freestyle Football Tanzania
Mandhari
Hongera kwa jaribio la kwanza! Basi ni vema usome Wikipedia:Mwongozo. BAdo kuna kasoro kadhaa kiumbo na ki-maelezo lakini usikate tamaa, chanzo ni kizuri!
- Uondoe MAANDISHO YOTE YA HERUFI KUBWA, iwe Maandishi ya Herufi Kubwa (kama ni jina...)
- mwanzoni pasiwepo kichwa yaani mstari inayoanza na kuishia kwa == ukifungua "hariri chanzo". Futa tu
- weka sehemu fupi ya maelezo ya msingi, halafu panga vichwa kufuatana na matini. Hapo ni sharti kueleza kifupi freestyle football ni kitu gani! (unaweza kuazima sentensi mbili kutoka simple:Freestyle_football, tafsiri au andika mwenyewe kwa Kiswahili)
- nashauri kufupisha kiasi kikubwa. Sehemu za Dira ya FFT, Dhamira ya FFT, Utawala ya FFT, Idara ya FFT na Vitengo vya FFT pamoja na madhumuni na majukumu sioni kuna habari zinazonielimisha. Sivyo ilhali ni klabu moja tu katika Tanzania hadi sasa vipengele hivi vinataja nia nzuri lakini hali halisi bado? Basi ningeshauri kuviacha nje tu.
- Vilevile Mipango - yaani wikipedia si mahali pa matangazo ya nia ya shirika kama hakuna hali halisi bado.
- LAKINI kama mmeshakuwa na mashindano - eleza kifupi kama ilikuwa ndani ya klabu tu, au kama wachezaji wa nje ya Dar au labda hata nje ya nchi walifika, au kama mlikuwa na wageni mmojammoja. Ila tu: Fupi.
- pia historia fupi: wangapi walianzisha na lini, iliandikishwa lini serikalini, idadi ya wanachama mwaka 2017, idadi ya wachezaji (ni wanachama = wachezaji?)
- Kama kulikuwa na taarifa ya magazeti, unaweza kutumia kama kiungo katika tanbihi
- Lazima ni kuweka jamii, nashauri uiingize katika Jamii:Mpira wa miguu
- Weka pia sehemu ya Marejeo, angalia mfano wa Mpira wa miguu
- Interwiki yaani kuunganisha na lugha nyingine nadhani haiwezekani maana kuhsu lemma hii hakuna makala nyingine bado.