Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Bilula

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bilula dhidi ya fauseti

[hariri chanzo]

Anja salaam. Ni tofauti gani kati ya bilula na fauseti? Ningependelea kutumia bilula kwa sababu ni neno la Kiswahili hasa. ChriKo (majadiliano) 10:45, 7 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Nimehamisha kwa bilula. Sioni ushahidi kwa kuwa "fauseti" ni Kiswahili. Pia sioni ushahidi kuwa ing. "faucet" ni tofauti na "tap" isipokuwa matumizi ya Mareka ni na ya Ki-Britania. Naona ni visawe tu. Kipala (majadiliano) 19:50, 12 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Fauseti ni tofauti na bilula kimuundo na utenda kazi. Fauseti huabatana na beseni (ya kuoshea mikono, kuoshea vyombo au kuogea mwili mzima) tofauti na bilula zingine. Fauceti huundwa kufunga na kufunguia maji ikimwaga kwa beseni bila maji kutapakaa. Tofauti pia ta bilula ya kawaida fauceti huchomoka kwa beseni ikiangalia juu tofauti na bilula ya kawaida inayo angalia upande. Ndio Fauceti ni uvumbuzi Malekani na ulifubuliwa kusahihisha makosa ya bilula za kawaida ambazo maji hutapakaa unapozitumia kwa beseni. Bilula ya kawaida pia haina uwezo wa fauceti wa kuzunguka kuangalia pande tofauti hivyo aiwezi tumika kkwa beseni zaidi ya moja tofauti na fauceti. --Anjakretfep (majadiliano) 09:26, 13 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Mpendwa naona unakaa sehemu ya Marekani ambako neno "faucet" inatumiwa kwa njia hii jinsi unavyoeleza. Lakini kabla ya kuleta habari ktk wikipedia heri ufanye utafiti kidogo kwanza. Faucet na tap ni visawe, labda moja zaidi Kimarekani nyingine zaidi Kibritania. Tena sijaona ushahidi kwa matumizi ya neno "fauseti" kwa Kiswahili. Naomba ulete. Wapi wanatumia neno hili? Tanzania angalau hamna. Wapi? Nairobi je? (sijawahi kusikia) Au kati ya watu wa Afrika ya Mashariki katika sehemu ya Marekani ulipo? Linganisha hapa, hapa na What are the differences between tap, faucet and spigot?. Kipala (majadiliano) 22:51, 13 Julai 2018 (UTC)[jibu]