Bilula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bilula ya shingo defu
Bilula
Bilula kwa ndani

Bilula (pia tapu ya maji, koki; ing. tap, faucet) ni aina ya valvu inayomwezesha mtumiaji kufunga na kufungulia maji yanayotoka kwenye bomba. Mara nyingi ni kifaa cha metali, kama vile chuma au shaba nyeupe lakini kuna pia za plastiki. Inafungwa mwisho wa bomba pale ambako maji huhitajika, kama vile kwenye mabeseni ya kuoshea vyombo jikoni au kunawia mikono, bafuni na kadhalika.

Bilula inajulikana tangu karne nyingi; haijulikani zilibuniwa wapi na lini lakini kuna mifano ya Roma ya Kale iliyohifadhiwa.

Kuna bilula za aina nyingi ukizingatia rangi, urefu, umbo, idadi ya vidude za kufungia na kufungulia maji, uwezo wake wakuzunguka kuangalia upande tofauti tofauti na utenda kazi.[1] [2] Bilula zingine zina uwezo wa kuchanganya maji kutoka bomba mbili tofauti kama vile maji yakutoka bomba la maji moto na maji baridi ya kutoka bomba ya maji baridi ili kuipatia anayetumia maji yenye joto anayotaka. Pia kuna bilula za kidijiti zenye vihisio digitali [3]za kufungulia na kufunga. Aina hizi za bilula hufungulia maji zenyewe punde tu mtu anapopitishia mkono karibu na kujifunga punde tu mtu anapotoa mikono.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Formisano, Bob (20 June 2018). The Different Types of Faucets (en-US). Iliwekwa mnamo 7 July 2018.
  2. Finch, Robert (23 December 2013). 14 Types of Kitchen Faucets You should Know Before You Buy (en-US). Iliwekwa mnamo 7 July 2018.
  3. Croll, David (19 May 2018). Best Kitchen Faucets – Make Your Kitchen Fancier (en-US). Iliwekwa mnamo 7 July 2018.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]