Majadiliano:Elisha mwankundile

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kawaida makala hii ningeifuta mara moja lakini nitaiacha siku 2 maana inaonekana kuna mgeni ambaye hajaelewa bado utaratibu. Nisipokosei ni Elisha mwenyewe aliyeandika hii. Ninamwomba ajiandikishe kama mtumiaji halafu yuko huru kujieleza jinsi anavyotaka kwenye ukurasa wake wa binafsi. Mwanafunzi kwa kawaida si mada ya makala - kama hakuna ushuhuda ya kwamba wamekuwa maarufu kwa sababu kitabu kimeandikwa juu yake au alikuwa mwenyewe sababu ya majadiliano katika jamii inayoonekana kwa njia ya magazeti n.k. Kama Elisha anajiandikisha atapata dirisha la Karibu lenye maelezo ya kimsingi Kipala (majadiliano) 15:19, 11 Mei 2012 (UTC)[jibu]

Naunga mkono hoja hii kwa nguvu zote. Umesema kweli kabisa, mzee wangu!--MwanaharakatiLonga 06:28, 12 Mei 2012 (UTC)[jibu]