Majadiliano:Barua ya kujiuzulu ualimu ya Julius Kambarage Nyerere

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Je makala hii ni kweli kuhusu barua ya kujiuzulu au kuhusu hotuba aliyotoa Nyerere? kwa bahati mbaya chanzo yaani blogu ya Mohamad Said haina habari za yale Nyerere aliandika katika barua yake na pia haina nukuu kutoka hotuba yake. Je matini hizi zinapatikana mahali? Ile picha siwezi kusoma kwa bahati mbaya.

Kuhusu kumtaja Padre Walsh nimeshangaa kidogo maana hadi sasa nimesikia tu huyu alikuwa mtu aliyempa Nyerere moyo ili aendelee na mwelekeo wake. Pia ya kwamba Nyerere aliendelea kutafuta ushauri wake. Sijakuta maelezo ya undani isipokuwa kumbukumbu ya padre mwingine Arthur H. Wille http://robertokanda.blogspot.de/2016/10/recollections-on-mwalimu-julius.html. Kufuatana na Wille tatizo ilikuwa madai ya serikali yaani gavana Twinings aliyelipa mishahara ya walimu wote hata wa shule za misioni kama Pugu. Lakini huyu ni mzee ambaye aliandika alichokumbuka na hii inaweza kuwa na makosa hasa kama hajatumia hati za kimaandishi. ingekuwa vema kama blogu ya Said ingetaja vyanzo kwa hitimisho yake. Kipala (majadiliano) 11:02, 2 Novemba 2016 (UTC)[jibu]

Nikifika nyumbani nitapakia picha inayoonekana vizuri ya Barua yake. Habari zinazowekwa humo nyingi anapata kwa wazee waliokuwa wa karibu sana na Nyerere. Nakumbuka picha hii alipewa na kina Issa Shivji, data na maelezo ya kina huwa anazungumza na watu wazito sana. Kuhusu makala aidha ya barua ya kujiuzuru au hotuba, Mzee Kipala, ilifika kipindi Nyerere alikuwa anatoa hotuba nzitonzito na hamasa juu ya Watanganyika. Ikumbukwe pia alikuwa anafanya kazi katika mashriki ya wakoloni, ulidhani viongozi wake wa hayo mashirika wangemuunga mkono? Haikuwa rahisi, ndiyo-maana alipata sapoti kubwa sana kutoka kwa Wazee wa Dar es Salaam kwa mshikamano wao. Soma makala ya Mshume Kiyate utaona urafiki wao na Nyerere. Kulikuwa na sababu zilizopelekea kujiuzuru ndiyo-maana tunataja mambo mengi kwa pamoja ili picha kamili ieleweke ya nini kilitokea.--MwanaharakatiLonga 13:26, 2 Novemba 2016 (UTC)[jibu]
Mzee Kipala, Sheikh Mohamed Said kaandika jibu: "Barua ya kujiuzulu Nyerere inapatikana na kama ilivyoelezwa hapa kuwa italetwa ili isomwe. Father Walsh kama mtumishi wa Kanisa alikuwa ni mshirika katika utawala wa kikoloni ambao TANU ilikuwa umeamua kuuondoa Tanganyika. Kwa vyovyote iwavyo asingeweza kumstahamilia Nyerere aipige vita serikali akiwa bado ni mtumishi wa Kanisa. Ieleweke kuwa Nyerere aliandika barua hiyo baada ya kurejea UNO ambapo sasa joto la kupinga ukoloni lilikuwa juu kiasi cha joto lile kutisha serikali na Kanisa. Muhimu si barua ya Nyerere ilikuwa na maneno gani. Barua ya kujiuzulu kazi haina filosofi yoyoye zaidi ya kueleza kusudio lake basi. Kuhusu Twining kulipa mishahara ya shule za Kanisa kuna paper muhumi sana katika kujua mchango wa serikali kwa shule za Kanisa kupitia kile kilichojulikana kama Grant-in- Aid kutoka serikalini (Angalia:http://www.muslimpopulation.com/africa/Tanzania/The%20Question%20of%20Muslim%20Stagnation%20in%20Education.php) Mohamed Said:The Question of Muslim Stagnation in Education (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Inter-cultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003)."

Tazama kisha mjibu. Naona kafungua akaunti kwa jina la Mwinyimadi...--MwanaharakatiLonga 14:20, 2 Novemba 2016 (UTC) [jibu]

Salamm Muddy, nitasubiri hadi barua ile inapatikana (wapi?)
Jinsi nilivyojifunza ni kweli kabisa ya kwamba huko mwanzoni walikuwa viongozi Waislamu wa pwani waliompokea Nyerere na kumpa nafasi aendelee kuwa kiongozi wa kitaifa. Pia inaonekana kabisa ya kwamba hali ya maendeleo kwa wanafunzi Waislamu baada ya uhuru haiwezi kuridhisha kabisa. Nakumbuka wakati nilipofanya kazi TZ kwenye miaka ya 1990-1993 kusoma mara kwa mara gazeti la An-Nur (? Jina?) ambako walionyehsa takwimu kuhusu idadi ya wanafunzi Waislamu kwenye ngazi za msingi, sekondari na yvuoni hadi asilimia ya walimu wa vyuo iliyokuwa mnamo 1-3 % nikikimbuka vema. Pia nimejifunza kidogo kuhusu uchungu uliokuwepo kati ya madhehebu wakati ule ingawa siasa ilihubiri "umoja" wakati wote.
Hata hivyo nina wasiwasi sana kuhusu picha blogu ile inachora kuhusu msimamo wa mapadre wazungu katika mazingira ya Mwalimu. Kumbukumbu katika mchango wa A. Wille niliyotuma (umeisoma?) ni tofauti sana, lakini blogu zote mbili hazileti vyanzo vya kutegemea. Je haiwezekani kuiona kinyume ya kwamba kuacha ualimu ilimweka Nyerere kuwa huru kuendesha shughuli za siasa? Angezunguka namna gani kama angepaswa kufundisha kila wiki? Si kweli ya kwamba Padre Walsh aliimpa Nyerere likizo kwenda New York ingawa gavana Twinings alijaribu kumzuia?
Pamoja na hayo bado nina swali kuhusu lemma ya makala hii - inayojadili jambo la maana sana. Basi najitahidi kutafuta vyanzo. Sawa? Kipala (majadiliano) 22:42, 3 Novemba 2016 (UTC)[jibu]
Endelea tu kutafuta vyanzo. ANGALIZO: Hutovipata kwa Waswahili isipokuwa katika makala za Wazungu wenzio ndiko wanakosema ukweli. Huku bwana kila kitu shaghalabaghala.. Pia nimeweka barua inayosomeka sasa! Wako...--MwanaharakatiLonga 17:06, 4 Novemba 2016 (UTC)[jibu]