Majadiliano:Akili bandia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ni akili "bandia" au "yakutengenezwa"[hariri chanzo]

Hivi naweza nikapewa elimu zaidi kuhusu matumizi ya neno "bandia" kama tafsiri ya neno "artificial"


Kwenye lugha ya kiswahili neno bandia ina maana sawa na neno "fake" kwenye kingereza

Yaani kitu cha "uongo" chenye dhumuni la kuhadaa au kutapeli, ni neno linaloibui hisia hasi.


Wakati "artificial" ni kile kilichoundwa na binadamu au kwa msaada wa binadamu.


Hofu yangu ni kuwa nahisi ni kosa kutumia neno bandia kama tasfiri ya neno "artificial" kwa sababu sio tafsiri sahihi ya kiswahili.


Alex Leo Tz (majadiliano) 11:53, 5 Desemba 2023 (UTC)[jibu]