Magret Hamisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Magret Hamisi Nzomiya

Magret Hamisi Nzomiya alizaliwa mnamo 1987 akapata elimu ya msingi kwenye shule ya Nyakato mkoani Mara. Alizaliwa katika familia ya Wazanaki ambao ni Wakristo.

Kazi yake ni kushona, uigizaji wa filamu nchini Tanzania.

Sanaa alianza toka alivyokuwa shule ya msingi, baada ya kumaliza shule alijiunga na vikundi mbali mbali vya sanaa, lakini hakubahatika kupata kikundi chenye msimamo. Mwaka 2008 alijiunga na kikundi cha Alwatan Artist Theatre chenye maskani yake Ilala. Alifaniwa majaribio na kuweza kupata nafasi ya kucheza sinema ya Bunge la wachawi. Katika sinema hiyo amecheza kama msichana mchawi anayeshirikiana na mama yake kuwafanyia ukatili mandondocha anayofuga mama yake.

Anasema kwa upande wa wasanii wa Tanzania anavutiwa muigizaji Mwajuma Abdul maarufu kama Maimuna.aliyecheza sinema ya uwanja wa dhambi. Kwa upande wa waigizaji wa nje ya Tanzania anavutiwa na Maria Clara anayecheza tamthilia ya Secret Diamor. Lengo ni kuwa msanii maarufu wa kimataifa. Anachukizwa na vitendo vya majungu, ugomvi, ubinafsi na umalaya vinavyofanywa na baadhi ya wasanii.