Nenda kwa yaliyomo

Maduka ya Army & Navy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Duka la House of Fraser,Westfield
uka la House of Fraser jijini Belfast

Maduka ya Army & Navy ni kundi la maduka ya nguo nchini Uingereza. Duka lao maarufu kabisa lilikuwa katika barabara ya Victoria Street jijini London, Uingereza.

House of Fraser ilinunua kundi hilo katika mwaka wa 1976. Duka hilo la Victoria Street liliuza bidhaa zake chini ya jina la Army & Navy,hadi mwaka wa 2005, lilipoitwa House of Fraser Victoria. Kila moja ya magorofa manne lina bidhaa mbalimbali kama nguo, mapambo,vipodozi, samani na vyombo vya kutumia umeme. 'Dunia ya Chakula', ukumbi mpya wa chakula katika maduka ya House of Fraser{ulioanzishwa jijini Birmingham katika mwaka wa 2003) ulifunguliwa katika gorofa la chini kabisa.Siku iyo hiyo walibadilisha jina la maduka haya kuwa 'House of Fraser'. Duka hilo linapatikana ndani ya Mji wa Wastminster, kusini mwa St. James' Park,hili ndilo duka la aina lake pekee katikamtaa huo.

Kampuni ya Iceland, Baugur, ilinunua House of Fraser mwishoni mwa mwaka wa 2006.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Duka hili lilianza kama muungano wa kijamii hasa muungano wa Army & Navy Co-operative Society ulioanzishwa na kundi la wanajeshi na wanamaji. Nia yao ilikuwa kuweza kueneza bidhaa za matumizi ya nyumbani na ya jumla kwa wanachama wao kwa bei nafuu sana. Duka lilifunguliwa katika kipande cha ardhi chicho hicho ambacho kinasimama hadi sasa mnamo 15 Februari 1872 kwa uuzaji wa mboga na likapanuliwa ili liweze kuhusu uuzaji wa bidhaa kama ngua, dawa na bunduki. Kufuatia mifumo ya muungano mbalimbali,kwa mfano muungano wa Civil Service Supply Association (Strand, London, 1864),muunganoo huu ulianza kutoa tikiti kwa wanachama wake kwa kila mwaka. Uanachama wa 'The Stores' ulijulikana kama kuwa wazi kwa wale waliokuwa katika vyeo vya juu katika jeshi ,wajane wa maafisa wa jeshi na wawakilishi wa mikahawa ya vikosi. Katika miaka ya baadaye,uanachama ulipanuliwa kuongeza watu wengi na tikiti zikatolewa bila malipo tangu mwaka wa 1922. Faida ya uanachama ilihusu malipo kutoka faida ya biashara hii na usafirishaji wa bure wa bidhaa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]