Mads Mikkelsen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mads Mikkelsen

Mads Mikkelsen, amezaliwa 22 Novemba 1965 mjini Copenhagen.
Amezaliwa Matthew Dittmann Michaelson
22 Novemba 1965
Kazi yake mwigizaji wa Denmark

Mads Mikkelsen (kwa (Kiingereza: Matthew Dittmann Michaelson; amezaliwa 22 Novemba 1965) ni mwigizaji wa Denmark.

Mikkelsen alizaliwa katika eneo la Østerbro, jijini Copenhagen. Baada ya kuhudhuria Shule ya Uigizaji ya Århus, ali filamu yake ya kwanza katika movie Pusher. Yeye ameigiza katika filamu maarufu za Kideni kama Flickering Lights (Kideni: Blinkende Lygter), The Green Butchers (Kideni: De Grønne Slagtere), na filamu yake ya kwanza Pusher, na Pusher II. Mikkelsen ameigiza katika jukumu maarufu la Askari katika kipindi cha Kideni cha Unit One (Kideni: Rejseholdet). Yeye pia aliigiza katika kipindi cha King Arthur kilichotayarishwa na Jerry Bruckheimer Tristan. Yeye pia aliigiza kama adui aitwaye Le Chiffre katika filamu ya 21 ya James Bond iitwayo, Casino Royale.

Mwaka wa 2008, Mikkelsen alialikwa na mtengezaji saa wa Uswizi aitwaye Swatch jijini Bregenz, Austria kwenye maonyesho ya Swatch 007 Villain Collection akiwa pamoja na adui wa James Bond mwingine, aitwaye Richard Kiel. Moja kati ya saa 22 imetengwa kwa "Le Chiffre", mchezaji kamari maarufu kwenye kipindi cha Casino Royale.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Runinga[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: