James Bond
James Bond ni mhusika aliyebuniwa na Ian Fleming mnamo 1953 kama mpelelezi wa Uingereza.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Miaka ya 1950 na 1960
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1953, Fleming ametunga Casino Royale, riwaya ya kwanza kabisa ya James Bond. Riwaya hiyo iliingiza hela kibao, na akaendelea kutunga riwaya moja ya James Bond kila baada ya mwaka mmoja hadi hapo alikuja-kufa mnamo 1963. Mnamo 1962 Albert. R. "Cubby" Broccoli na Harry Saltzman wakaanza kutayarisha filamu ya kwanza ya James Bond, Dr. No, ndani yake anakuja Sean Connery akicheza kama James Bond. Filamu ikawa maarufu mno, na wakaendelea kutengeneza filamu nyingine nyingi tu za Bond. Mwishoni mwa miaka ya 1960, Connery hakutaka tena kuendelea kucheza filamu za Bond, na wengi wakafikiria kwamba Bond sasa amekufa. Mnamo 1969, George Lazenby ameonekana katika filamu moja akiwa kama Bond, lakini filamu haikupata mafanikio.
Miaka ya 1970 na 1980
[hariri | hariri chanzo]Kunako miaka ya 1970, watayarishaji wakaibuka na filamu ya Live and Let Die, ndani yake anakuja Roger Moore akiwa kama Bond. Filamu ikapata mafanikio makubwa sana. Mfululizo huo uliendelea hadi katika miaka ya 1970 na 1980 na Roger Moore anaendelea kucheza kama Bond.
Kunako miaka ya 1980, filamu za Bond hazikuwa zenye mafanikio sana kama jinsi zilivyokuwa. Tofauti na zile za miaka ya 1960 na 1970, kwenye miaka ya 1980 kulikuwa na filamu nyingi za kupigana ambazo zilikuwa nzuri kupita hata mifululizo ya Bond.
Baada ya Moore kuachia nafasi ya kucheza kama Bond, nafasi yake ilishikiriwa na Timothy Dalton mwishoni mwa miaka ya 1980. Dalton alijaribu kukaza zaidi, "uhalisia wa mambo" Bond, ilikaribiana kabisa na riwaya za Fleming. Washabiki hawakuvutiwa na tafsiri ya uhusika wa Bond uliofanywa na Dalton, na kwa maana hiyo filamu ikaiingiza hela mbuzi.
Miaka ya 1990
[hariri | hariri chanzo]Vita Baridi imeisha mnamo mwaka wa 1991. Kwa kuwa uhusika wa Bond kiduchu hupiagana dhidi ya Ukomunisti, wengi walifikiria kwamba mfululizo wa filamu za Bond sasa umekufa jumla.
Kunako 1995, watayarishaji wakatengeneza filamu ya Goldeneye, ndani yake anakuja Pierce Brosnan akiwa kama Bond. Filamu hii imefanya uhusika wa Bond ujulikana kupitiliza katika miaka ya 1990. Brosnan ameoana katika filamu kadhaa za Bond.
Miaka ya 2000
[hariri | hariri chanzo]Kunako 2002, uhusika wa James Bond ulitumika katika filamu ya ishirini ya Die Another Day, maadhimisho ya 40 ya mfululizo wa filamu hizi na maadhimisho ya 50 tangu Fleming ametunga riwaya yake ya kwanza ya Bond. Mnamo 2006, filamu ya 21, Casino Royale, ilitolewa. Pierce Brosnan, ambaye ailicheza katika filamu tano za awali za James Bond, alibadilishwa na Daniel Craig, James Bond wa kwanza kuwa na nywele za manjano. Filamu inatokana na riwaya ya kwanza ya Ian Fleming ambayo ina jina sawa na hili la filamu, lakini yenyewe ipo katika maisha ya sasa. Filamu imemwonesha Richard Branson, bilionea wa Kiingereza na modeli mpya ya Aston Martin DB9, gari ambalo lilimpa sifa sana James Bond katika miaka ya 1960. Washabiki wengi wanadhani kwamba filamu hii ipo tofauti na zile nyingine, hii ni bora zaidi, na filamu hizo za baadaye (ingawa zitakuwa chache) huenda zikawa kwenye muundo mpya. Mnamo 2008, Craig ameonekana katika filamu ya pili ya Bond, Quantum of Solace.
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Filamu nyingi za James Bond zilikuwa bab-kubwa. Hata hivyo, kuna filamu mbili ambazo ziliainishwa kama sio mfululizo rasmi wa filamu Bond na wala hazitambuliki kama moja ya sehemu ya mfululizo. Filamu hizo ni pamoja na toleo la 1967 la Casino Royale ilibuma, imemshirikisha "Jimmy Bond". Pia, Never Say Never Again haikutengenezwa na kampuni ya Albert R. Broccoli, EON Productions.