Mabel Wheeler Daniels

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mabel Wheeler Daniels (Swampscott, Massachusetts, 27 Novemba 1878 - Boston, 10 Machi 1971) alikuwa mtunzi wa nyimbo, kiongozi wa kwaya, na mwalimu nchini Marekani. Alisoma Chuo cha Radcliffe akijifunza pamoja na George Whitefield Chadwick kabla ya kusafiri kwenda Munich huko Ujerumani kwa ajili ya kujifunza zaidi. Aliporudi Marekani akawa mkuu wa idara ya muziki katika Chuo cha Simmons, hadi mwaka 1918. Aliendelea kufanya kazi mpaka mwishoni mwa maisha yake, na alitunukiwa shahada za heshima na Chuo Kikuu cha Boston na Chuo Kikuu cha Tufts.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Enchantment, op. 17, no. 1, (1908)" by Mabel Wheeler Daniels" In Library of Congress
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mabel Wheeler Daniels kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.