Nenda kwa yaliyomo

Maambukizi ya virusi vya papilloma vya binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maambukizi ya virusi vya papilloma vya binadamu
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuMagonjwa ya kuambukiza, Jinakolojia, Onkolojia
DaliliHakuna, uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi[1][2]
VisababishiVirusi vya papilloma vya binadamu husambaa kwa njia ya mgusano wa moja kwa moja[3][4]
KingaChanjo za HPV, kondomu, mwenza mmoja maishani, kutofanya ngono[5][6]
Idadi ya kutokea kwakeWatu wengi wameambukizwa na HPV wakati fulani katika maisha yao[3]

Maambukizi ya virusi vya papilloma vya binadamu (Human papillomavirus infection, yaani HPV) ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya papilloma vya binadamu.[4]

Takriban 90% ya maambukizo ya ugonjwa huu hayasababishi dalili zozote na huisha yenyewe ndani ya miaka miwili.[1] Hata hivyo, katika baadhi ya matukio, maambukizi ya ugonjwa huu yanaendelea na kusababisha aidha uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi au vidonda vya awali vya saratani.[2] Vidonda hivi, kulingana na eneo lililoathiriwa, huongeza hatari ya saratani ya mlango wa kizazi cha wanawake, uke (vagina), uke (vulva), uume, mkundu, mafindo au koo.[1][2] Takriban saratani yote ya mlango wa kizazi cha wanawake inatokana na ugonjwa huu; aina mbili, HPV16 na HPV18, huchukua 70% ya hali hazi.[1][7] Kati ya 60% na 90% ya saratani zingine zilizoorodheshwa hapo juu pia zinahusishwa na HPV.[7] HPV6 na HPV11 ni sababu za kawaida za uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi ya uzazi na papilomatosisi ya koo (laryngeal papillomatosis).[1]

Maambukizi ya HPV husababishwa na virusi vya papilloma vya binadamu, virusi vya DNA kutoka kwa familia ya papillomavirus.[8] Zaidi ya aina 170 zimeelezewa.[8] Zaidi ya aina 40 zinaweza kuenea kwa njia ya kujamiiana na kuambukiza njia ya haja kubwa na sehemu za siri.[3] Sababu za hatari kwa maambukizo ya mara kwa mara na aina za zinaa ni pamoja na umri mdogo wa kujamiiana kwa mara ya kwanza, wenzi wengi wa ngono, uvutaji sigara, na utendaji duni wa kingamwili.[1] Aina hizi kwa kawaida huenezwa kwa mgusano endelevu wa moja kwa moja wa ngozi hadi ngozi, huku ngono ya uke na njia ya haja kubwa ikiwa ndiyo njia inayojulikana zaidi. [3] Pia, maambukizi ya HPV yanaweza kuenea kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa ujauzito.[9] Hakuna ushahidi kwamba HPV inaweza kuenea kupitia vitu vya kawaida kama vile viti vya choo,[10] lakini aina zinazosababisha uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi zinaweza kuenea kupitia maeneo kama vile sakafu.[11] Mtu anaweza kuambukizwa na aina zaidi ya moja ya HPV.[9] HPV inajulikana kuathiri wanadamu pekee.[4][12]

Chanjo za HPV zinaweza kuzuia aina za kawaida za maambukizi.[3] Ili kuwa na ufanisi zaidi, chanjo inapaswa kutumika kabla ya kuanza kwa shughuli za ngono, na kwa hivyo inashauriwa kati ya umri wa miaka 9-13.[1] Matumizi ya mara kwa mara ya kondomu ya kiume yanaweza kupunguza maambukizi ya HPV ya wanawake kwa karibu 70%, ingawa maeneo ambayo hayajafunikwa yanaweza kuambukiza eneo la nje la uke.[5][6] Kuwa na mke mmoja maishani, au kujizuia kufanya ngono kunaweza kupunguza maambukizi ya HPV ya sehemu za siri.[5] Uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi cha wanawake, kama vile mtihani wa Papanicolaou ("pap smear"), au uchunguzi wa seviksi baada ya kupaka asidi asetiki (acetic acid), unaweza kugundua saratani ya mapema na seli zisizo za kawaida ambazo zinaweza kuibuka na kuwa saratani.[1] Uchunguzi huruhusu matibabu ya mapema ambayo husababisha matokeo bora.[1] Uchunguzi umepunguza idadi ya kesi na idadi ya vifo kutokana na saratani ya mlango wa kizazi cha wanawake.[13] Uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi unaweza kuondolewa kwa kugandisha (freezing).[4]

Karibu watu wote wameambukizwa na HPV, wakati fulani katika maisha yao.[3] HPV ndio maambukizo ya zinaa (STI) ya kawaida zaidi ulimwenguni.[5] Ulimwenguni kote mnamo 2018, inakadiriwa matukio mpya 569,000 ya saratani ya shingo ya kizazi zilitokea, na vifo 311,000.[14] Takriban 85% ya saratani hizi za shingo ya kizazi zilitokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.[1] Nchini Marekani, takriban matukio 30,700 ya saratani kutokana na HPV hutokea kila mwaka.[15] Takriban, 1% ya watu wazima wanaofanya ngono, wana vidonda vya sehemu za siri.[9] Matukio ya uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi yameelezewa tangu wakati wa Ugiriki ya kale, wakati ukweli kwamba hivyo husababishwa na virusi ulijulikana mwaka wa 1907.[16]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 "Human papillomavirus (HPV) and cervical cancer". WHO. Juni 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Ljubojevic S, Skerlev M (2014). "HPV-associated diseases". Clinics in Dermatology. 32 (2): 227–34. doi:10.1016/j.clindermatol.2013.08.007. PMID 24559558.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 "What is HPV?". CDC. 28 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Milner, Danny A. (2015). Diagnostic Pathology: Infectious Diseases. Elsevier Health Sciences. uk. 40. ISBN 9780323400374. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2017.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 Nakra, Natasha A.; Blumberg, Dean A. (2022). "16. Human Papillomavirus infections and prevention". Katika Jong, Elaine C.; Stevens, Dennis L. (whr.). Netter's Infectious Diseases (kwa Kiingereza) (tol. la 2nd). Philadelphia: Elsevier. ku. 71–74. ISBN 978-0-323-71159-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 2 Oktoba 2023.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 "Fact Sheet for Public Health Personnel | Condom Effectiveness | CDC". www.cdc.gov. 25 Machi 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Mei 2017. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 "The Link Between HPV and Cancer". CDC. Septemba 30, 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Novemba 2015. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 Bzhalava D, Guan P, Franceschi S, Dillner J, Clifford G (Oktoba 2013). "A systematic review of the prevalence of mucosal and cutaneous human papillomavirus types". Virology. 445 (1–2): 224–31. doi:10.1016/j.virol.2013.07.015. PMID 23928291.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. 9.0 9.1 9.2 "Human Papillomavirus (HPV) Questions and Answers". CDC. 28 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "5 Things You Might Not Know About Human Papillomavirus". CDC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Human Papilloma Virus (HPV)" (PDF). WRHA. 18 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 26 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Pink Book (Human Papillomavirus)" (PDF). CDC.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 21 Machi 2017. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. Sawaya GF, Kulasingam S, Denberg TD, Qaseem A (Juni 2015). "Cervical Cancer Screening in Average-Risk Women: Best Practice Advice From the Clinical Guidelines Committee of the American College of Physicians". Annals of Internal Medicine. 162 (12): 851–9. doi:10.7326/M14-2426. PMID 25928075.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Global Cancer Observatory: International Agency for Research on Cancer" (PDF). IARC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 11 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. Viens LJ, Henley SJ, Watson M, Markowitz LE, Thomas CC, Thompson TD, na wenz. (Julai 2016). "Human Papillomavirus-Associated Cancers - United States, 2008-2012". MMWR. Morbidity and Mortality Weekly Report. 65 (26): 661–6. doi:10.15585/mmwr.mm6526a1. PMID 27387669.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. Tyring, Stephen; Moore, Angela Yen; Lupi, Omar (2016). Mucocutaneous Manifestations of Viral Diseases: An Illustrated Guide to Diagnosis and Management (tol. la 2nd). CRC Press. uk. 207. ISBN 9781420073133. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2020.