Ujuzi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumbnail|300px|Mwanafalsafa Francis Bacon alisema "Ujuzi ni mamlaka" ("knowledge is power") '''Ujuzi'''maana yake ni kufahamu, ku...'
 
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:Francis Bacon 2.jpg|thumbnail|300px|Mwanafalsafa Francis Bacon alisema "Ujuzi ni mamlaka" ("knowledge is power")]]
[[Picha:Francis Bacon.jpg|thumbnail|300px|Mwanafalsafa Francis Bacon alisema "Ujuzi ni mamlaka" ("knowledge is power")]]
'''Ujuzi'''maana yake ni kufahamu, kujua na kuelewa hali, habari na maelezo yanayohusu mazingira tunapoishi. Tunapata ujuzi kwa maarifa yetu au kwa njia ya kufundishwa tukitazama, kutambua, kulinganisha na kutafakari yale tuliyoona na kujifunza.
'''Ujuzi'''maana yake ni kufahamu, kujua na kuelewa hali, habari na maelezo yanayohusu mazingira tunapoishi. Tunapata ujuzi kwa maarifa yetu au kwa njia ya kufundishwa tukitazama, kutambua, kulinganisha na kutafakari yale tuliyoona na kujifunza.



Pitio la 18:55, 9 Machi 2015

Mwanafalsafa Francis Bacon alisema "Ujuzi ni mamlaka" ("knowledge is power")

Ujuzimaana yake ni kufahamu, kujua na kuelewa hali, habari na maelezo yanayohusu mazingira tunapoishi. Tunapata ujuzi kwa maarifa yetu au kwa njia ya kufundishwa tukitazama, kutambua, kulinganisha na kutafakari yale tuliyoona na kujifunza.

Kimsingi tunaona tofauti kati ya ujuzi na rai au hoja tupu. Rai na hoja zinakuja pamoja na hisia na maarifa ambayo mara nyingi haikutafakiriwa kimakini. Kinyume chake ujuzi ni yale tunayoona kuwa una kiwango kikubwa cha uhakika baada ya kujadiliwa na watu wengi katika mchakato unaoeleweka. Lakini kila ujuzi una kiwango cha kukosa uhakika kwa sababu uwezekano wa makosa katika kuelewa halisia unabaki kila wakati.

Katika falsafa elimu jinsi ya kupata ujuzi huitwa epistomolojia. Mwanafalsafa Plato alieleza ujuzi kuwa "rai ya kweli yenye msingi mzuri" (englisch justified true belief).