Kunona : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Badiliko: eu:Gizentasun
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: ga:Murtall
Mstari 83: Mstari 83:
[[fiu-vro:Lihonõminõ]]
[[fiu-vro:Lihonõminõ]]
[[fr:Obésité]]
[[fr:Obésité]]
[[ga:Murtall]]
[[gl:Obesidade]]
[[gl:Obesidade]]
[[he:השמנת יתר חולנית]]
[[he:השמנת יתר חולנית]]

Pitio la 21:07, 4 Februari 2012

Mtajiri mwenye kunona kwenye picha ya karne ya 17

Kunona ni hali ya mwili kuwa mnene na mzito mno. Neno la mganga ni "adipositas". Kipimo chake ni uhusiano kati ya urefu wa mtu na uzito wake.

Magonjwa yanayotokana na kunona

Kuwa mneme mno kiasi cha kunona kunaleta hatari ningi za kiafya na kusababisha magonjwa kama vile

  • Shinikizo la juu la damu
  • Ugonjwa wa kisukari
  • Ugonjwa wa moyo
  • Kupooza
  • Shida za kupumua
  • Matatizo ya viungo vya miguu na kwenye uti wa mgongo

Watu wanaonona hufa mapema na kuwa na magonwa yningi kuliko watu wembamba wanaokula kiasi jinsi wanavyohitaji chakula.

Sababu za uenezaji kwa kunona

Sababu za kimsingi wa kunona ni kula chakula kingi tena chakula chenye mafuta mengi na kutofanya mazoezo ya kimwili wa kutosha. Kunona kilitokea wakati wote katika historia lakini siku hizi imekuwa tatizo kubwa sana kwa sababu ya mabadiliko ya maisha.

Watu hunenepa kupita kiasi hasa kutokana na sababu kama vile

  • katika mazingira maskini ambako kuna watu wenye njaa kunenepa kunaonekana kama dalili ya kufaulu maishani na ya uwezo
  • watu wanafuata uzoefu wa chakula uliotokea zamani ambako watu wote walifanya kazi mashambani lakini wakati huu hawafanyi tena kazi nzito ya kimwili ila tu wanaendelea kula chakula kingi na kizito kama mababu
  • watu wanaofanya kazi ofisini wakiketi siku yote lakini hawana kazi ya kimwili
  • watu wanaozunguka kwa gari tu au usafiri lakini hawatembei tena
  • watu wanaotumia muda wao nyumbani wakiketi tena ama mbele ya runinga au mbele ya kompyuta
Mtu wa kunona sana

Kipimo cha kunona

Madaktari wanatumia mbinu mbalimbali kukadiria kiasi cha kunona. Kile kinachotumiwa zaidi ni mkadirio ya kipeo cha masi ya mwili (body mass index). Hapa uzito wa mtu mzima hugawiwa kwa mraba wa urefu wake kwa mita.

Kwa mfano mtu mwenye urefu wa 1.71 mita anazidisha 1.71 kwa 1.71 = 2,9241. Akiwa na uzito wa kilogramu 70 hesabu ni 70 : 2,92 = 24,6. Ile 24,6 ni namba ya kipeo cha masi ya mwili chake.

Madaktari husema: kama kipeo hiki kipokati ya 18.5 na 25 mtu huyu ana uzito sawa kabisa. Akiwa na kipeo cha masi ya mwili kati ya 25 na 30 anahesabiwa uwa mnene. Akizidi 30 ananona na akizidi 35 ananona sana na hiki ni kiwango cha hatari kubwa kwa afya.

Kwa mfano wa mtu wetu mwenye urefu wa mwili wa 1.71 mita bado yuko sawa akiwa na kilogramu 73. Akizidi uzito wa 73 kg anaonekana mnene kiasi au zaidi. Kuanzia uzito wa kilogramu 87 daktari atamwambia "Sasa unanona". Akifikia kilogramu 102 ameshanona sana.


Kuzuia au kupunguza kunona

Watu wanashauriwa kubadilisha uzoefu wao wa chakula pamoja na uzoefu wao wa kazi ya kimwili. Tiba hii si vigumu lakini ugumu wake ni moyo wa mtu yaani udhaifu wa watu wanaoshaindwa mara nyingi kubadilisha kawaida yao.

Kuhusu chakula ni vema kuangalia kile tunachokula na kile tunachoacha. Ni vema kuacha au kupunguza sana vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi kama vile chipsi, biskuti, peremende, siagi, majarini, kachumbari, chumvi, vyakula vilivyokaangwa, aiskrimu na soda yenye sukari. Pia kula vyakula vidogo ambavyo vimekaangwa au vilivyo na wanga.

Kinyume chake ni vema kula matunda na mboga majani. Tena kula mara nyingi kidogokidogo kuliko kushiba sana wakati moja.

Kuhusu mazoezi kama kazi yetu ni ya kuketi tunshauriwa kufanya kazi ya kimwili kama mazoezi, michezo au kutembea haraka kwa angalau nusu saa mara tatu kila wiki hadi kutoa jasho.


Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA