Sheria : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: kn, sr Ondoa: sg Badiliko: sc
d roboti Nyongeza: mwl:Dreito
Mstari 87: Mstari 87:
[[mk:Право]]
[[mk:Право]]
[[ms:Undang-undang]]
[[ms:Undang-undang]]
[[mwl:Dreito]]
[[ne:कानून]]
[[ne:कानून]]
[[nl:Recht]]
[[nl:Recht]]

Pitio la 01:44, 22 Septemba 2009

Neno la Sheria lina asili ya Kiarabu (شريعة Shari'ah) na kulingana na Kamusi ya Kiswahili Sanifu, iliyotolewa na TUKI (Dar es Salaam), Sheria ni:

A)

1) amri zinazotungwa na bunge la nchi fulani ili kusimamia taratibu za nchi hiyo na ambazo ni lazima zifuatwe na watu waliomo humo na anayekwena kinyume nazo hupewa adhabu na mahakama.

2) kanuni zinazotungwa na chombo kama vile halmashauri, na kadhalika kilichopewa mamlaka na bunge ili kusimamia taratibu za mahali fulani kama vile mji, kampuni, mashirika, na kadhalika.

3) sheria za mila ambazo ni kanuni zinazoendesha taratibu za jamii au kabila fulani ambazo aghalabu hutumika ili kuleta suluhu badala ya kutoa adhabu.

B)

- kanuni zinazoendesha taratibu za maisha ya waumini wa dini fulani na ambazo zinatoka Mwenyezi Mungu.

Makala inayofuata imeandikwa kulingana na itikadi ya kidini kwa hiyo inafuata maelezo B.

Mara nyingi neno sheria hutumika kwa maana ya Kanuni katika mazungumzo ya kawaida, lakini Sharia hasa ni hukumu alizoziteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume na Manabii kunadhimu maisha ya wanadamu hapa duniani. Ama Kanuni, huwa ni hukumu zilizopangwa na wanadamu kuendesha maisha yao katika mambo ambayo Sharia haikugusia.

Sharia tofauti na Itikadi (Imani) ambayo ni thabiti, ni jambo linalokuwa na kubadilika kwa mujibu wa wakati na zama mbali mbali na huwa inalingana na mazingira ya watu wanapoishi. Mitume waliletwa kwa wanadamu na kuletewa Sharia ili waweze kudhibiti maisha ya jamii zao, kusikuwepo na dhulma wala kukiuka mipaka.

Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu aliweka mipaka ya kila kitu na kufafanua kwa wanadamu mipaka hii ili wasiipindukie. Ikawa kila jambo katika maisha ya binadamu lina mpaka wake: Chakula mwanadamu ameruhusiwa kula vitu vingi sana, lakini amewekewa mipaka asile vitu fulani, wala asifanye israfu na ubadhirifu katika kula. Ndoa aoe anayempenda katika wanawake, lakini watu aina fulani hawezi kuwaoa, wala kupindukia idadi fulani, wala kukaa na wakeze bila kufanya uadilifu.

Hii ni mifano ya mipaka, na mipaka kama hii iko katika kila sehemu ya maisha ya mwanadamu, ili watu katika jamii waishi kwa maskilizano, wema na hisani, bila ya kuudhiana wala kukerana.