Jamhuri ya Bou Regreg : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d - sw
Mstari 13: Mstari 13:
[[fa:ابی رقراق]]
[[fa:ابی رقراق]]
[[fr:Bouregreg]]
[[fr:Bouregreg]]
[[sw:Bou Regreg]]

Pitio la 14:52, 19 Desemba 2006

Jamhuri ya Bou Regreg ilikuwa dola ndogo katika eneo la miji Rabat na Sale mdomoni wa mto Bou Regreg lililoanzishwa mwaka 1627. Watwala walikuwa maharamia waliounda serikali baada ya mwisho wa utawala wa ufalme wa Wasaadi.

Halmashauri ya wawakilishi iliwateua nahodha mkuu kwa ajili ya jahazi za haramia na pia magavana wa Rabat na Sale. Maharamia walishambulia hasa jahazi za nchi za Wakristo. Miji yote miwili ikatajirika na majengo mengi ya kitovu cha kihistoria ya Rabat yalijengwa wakati ule. Mwaka 1668 wenyeji walipaswa kukubali utawala wa wafalme Waalawi lakini hali halisi waliendelea kujitegemea hadi mwaka 1818.