Louis XIV wa Ufaransa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Louis XIV

Louis XIV (5 Septemba 1638- 1 Septemba 1715) alikuwa mfalme wa Ufaransa tangu 14 Mei 1643 hadi kifo chake.

Alikuwa mfalme kwa umri wa miaka minne akakabidhiwa madaraka alipotimiza miaka 21.

Louis alilenga kuunganisha mamlaka yote mkononi mwake. Alisimamia shughuli za serikali na mawaziri wote walitakiwa kutoa ripoti moja kwa moja kwake. Alitumia mapato yote ya taifa kama mapato yake mwenyewe akiamua peke yake. Alivunja upinzani wa waungwana na kuimarisha utawala wa serikali kuu katika milki yake. Alijenga uchumi wa nchi na kuendesha siasa ya nje iliyofanya Ufaransa kuwa taifa kiongozi katika Ulaya.

Katika siasa ya ndani alimaliza Sheria ya Nantes ulioruhusu uhuru wa kidini akapiga Uprotestanti marufuku na kudai watu wote wasali katika kanisa katoliki. Waprotestanti Wafaransa 200,000 waliondoka katika nchi wakikimbia Ujerumani hasa Prussia na Uingereza.

Alitumia pesa nyingi kwa ujenzi ya majumba ya kifalme hasa jumba kubwa la Versailles. Alianzisha pia taasisi za sayansi na sanaa. Utamaduni wa Ufaransa ulikuwa kielelezo kwa nchi za Ulaya.

Katika vita zake alipanusha milki yake kwa kutwaa maeneo yaliyokuwa chini ya Hispania, Ujerumani na Uholanzi.

Aliacha urithi wa muundo wa utawala ambako mfalme alikuwa sawa na dola na serikali.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Louis XIV wa Ufaransa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.