Loïc Gasch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Loïc Gasch (amezaliwa 13 Agosti 1994) ni mwanariadha wa mchezo wa kuruka juu kutoka nchini Uswisi. Alimaliza nafasi ya kumi katika mashindano ya Uropa ya mwaka 2018. Aliwahi kushiriki katika mashindano ya U23 ya Uropa ya mwaka 2015 na kushindwa kufika fainali.

Urukaji wake bora ni mita 2.26 aliyoifikisha julai 2017 huko Zurich, kabla ya kuruka mita 2.33 ambayo ndiyo rekodi yake mpya aliyoiweka huko Stade olympique de la Pontaise, Lausanne nchini Uswisi mnamo 8 Mei 2018.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Loïc GASCH | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-12.