Lieb Bester

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lieb Bester
Amezaliwa Aprili 15,1949
Brakpan, Transvaal, Afrika Kusini
Amekufa Julai 21,2021
Pretoria, Gauteng, Afrika Kusini
Kazi yake Mwigizaji, Mwanamuziki

Lieb Bester 15 Aprili 1949 - 21 Julai 2021 alikua mwanamuziki na muigizaji wa filamu kutokea nchini Afrika Kusini. Alijulikana sana kwa umashuhuri wake katika jukumu kubwa la Fritz Retief ndani ya kykNET katika mfululizo wa vipindi vya televisheni vilivyokua vikichukuliwa na kurushwa hewani kila siku vilivyojulikana kama Villa Rosa. Kutokana na jukumu hili, alishinda tuzo ya ATKV Media Veertjie ya Muigizaji Bora katika maigizo ya vipindi vilivyorushwa kila siku mnamo 2012 na 2013.[1]Bester pia alijulikana kwa jukumu lake kama msimamizi mwandamizi George Lindeque katika tamthiliya ya Televisheni ilijulikana kwa jina la Arsenal, ambayo awali ilitangazwa kwenye SABC2.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Bester alizaliwa mnamo 15 Aprili 1949 huko Brakpan na kusajiliwa kama mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Stofberg mnamo 1967. Baada ya shule, alifanya miezi tisa ya utumishi wa lazima wa kijeshi huko Walvis Bay. Alicheza kwanza mnamo 1969 kama mwigizaji katika mchezo wa Die Ryk Weduwee van Uys Krige. Filamu yake ya kwanza ilikuwa Seun van die Wildtemmer mnamo 1973. Bester alicheza vyombo vya muziki anuwai, pamoja na piano, kibodi, akodoni, kinanda na gita. Alikuwa sehemu ya kikundi cha wacheza densi waliojulikana kama Take 3, pamoja na wenzake wawili, yani Jan Coetzer na Deon Heyneke.[2][3]

Kazi ya kijeshi[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 1978 Bester alikuwa mwanachama wa jeshi la Afrika Kusini na alistaafu mnamo mwaka 2001 akiwa na cheo cha kanali. Wakati wa huduma yake, alifanya kazi katika vitengo vifuatavyo:

  • Makao Makuu ya Jeshi (Pretoria) 19781980;
  • Kikosi cha 7 cha Wanajeshi wa nchi kavu (Phalaborwa) 19811982;
  • Shule ya Wanajeshi watembeao kwa mguu/nchi kavu (Oudtshoorn) 19831986;
  • SWA Kituo cha utawala wa Mkoa (Windhoek) 1987–1989;
  • Amri Makao Makuu ya Natal (Durban) 1989–1990;
  • Makao Makuu ya Kamandi ya Mkoa wa Magharibi (Cape Town) 1991–1992;
  • Huduma ya Afya ya Kijeshi ya Afrika Kusini Makao Makuu (Centurion) 1993–1995;
  • Chuo cha Huduma ya Afya ya Jeshi la Afrika Kusini (Voortrekkerhoogte) 1996–1997;
  • Usalama wa Kijeshi (Pretoria) 1998–2001.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Bester aliiaga dunia mnamo Julai 21, 2021, baada ya kulazwa hospitalini kwa mara ya pili kwa sababu ya UVIKO-19. Aliiaga Dunia akiwa na umri wa miaka 72.[4]

Filamu Shiriki[hariri | hariri chanzo]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

  • Stof (filamu fupi) (2003)
  • Stander (filamu)|Stander (2003), kama msomaji habari wa Televisheni
  • Panic Mechanic (1996), kama Gys
  • Agter Elke Man (1990), kama Reinders
  • Savage Encounter, 1980
  • Die Rebel (1976), kama Wakala wa Kijerumani
  • Liefste Madelein (1976)
  • Hank, Hennery en Vriend (1976), kama Hennery
  • Jakkalsdraai se Mense (1975)
  • Mirage Eskader, (1975) kama Martin Bekker
  • Ses Soldate, (1974) kama Liebling
  • Skadu's van Gister, (1974)
  • Seun van die Wildtemmer, (1973)

Televisheni[hariri | hariri chanzo]

  • Met 'n Huppel in Die Stap (2018–2021), kama mtoa huduma wa eneo (kykNET)
  • Villa Rosa (2005–2015), kama profesa Fritz Retief (kykNET)
  • Sterk Skemer kama (Maj.) Balt Otto
  • Arsenaal, kama msimamizi mwandamizi George Lindeque (SABC2)
  • Kriminele Meesterbrein (2003), kama mtoa huduma wa eneo (kykNET)
  • Ietermagô (2002), kama Bulla Sonnekus
  • Justice for All (1998), kama Dries Alberts
  • Soldier Soldier (BBC) (1995), kama Luteni kanali Danie Reitz
  • Paradys (Miendelezo ya Tamthilia katika Televisheni), 1994
  • Opdrag
  • TJ 7
  • Phoenix en Kie
  • Dis Koud Hier

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "kykNET programme blink uit by die ATKV-Mediaveertjies". kykNET. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-25. Iliwekwa mnamo 2021-10-09. 
  2. "Profiel op tvsa.co.za". tvsa.co.za. 
  3. "Profiel op Who's Who SA". Who's Who SA. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-19. Iliwekwa mnamo 2021-10-09. 
  4. Ferreira, Thinus. "Veteran actor Lieb Bester (72) dies", 21 July 2021. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lieb Bester kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.