Liam Payne
Liam James Payne (29 Agosti 1993 – 16 Oktoba 2024) alikuwa mwimbaji wa Uingereza. Alijulikana zaidi kama mshiriki wa kundi la muziki wa pop la wavulana, One Direction, ambalo lilikuwa mojawapo ya makundi ya muziki wa wavulana yaliyouza zaidi ya wakati wote.
Payne alijaribu kushiriki kwenye kipindi cha runinga cha Uingereza, The X Factor mwaka 2008, lakini ni mwaka 2010 baada ya kujaribu tena ndipo alipowekwa kwenye kundi na washiriki wengine wanne ili kuunda One Direction. Kundi hilo lilipata mafanikio makubwa duniani kabla ya kujiweka kando mwaka 2015.
Baada ya kundi hilo kwenda mapumzikoni, Payne alianza kazi ya muziki kama msanii wa kujitegemea, akisaini mkataba na Republic Records kwa ajili ya Amerika Kaskazini. Mnamo mwaka 2017, alitoa wimbo wake wa kwanza kama msanii wa pekee, "Strip That Down", ambao ulifika nafasi ya tatu kwenye Chati za Uingereza (UK Singles Chart) na nafasi ya kumi kwenye chati za Marekani (US Billboard Hot 100), na ukapata cheti cha platinum katika nchi zote mbili. Albamu yake ya kwanza, LP1, ilitolewa Desemba 2019. Katika miaka mitatu ya mwanzo ya kazi yake ya pekee, Payne aliuza zaidi ya nyimbo milioni 18, albamu milioni 2.4, na alipata zaidi ya mamilioni 3.9 ya kusikilizwa kwenye majukwaa ya mtandao.
Mbali na kazi yake ya kibinafsi, Payne pia alitayarisha remixes kwa majina ya utani "Big Payno" na "Payno". Alishirikiana na wasanii wengine na kutengeneza remixes za nyimbo za kundi lake pamoja na mwimbaji Cheryl.
Payne alifariki tarehe 16 Oktoba 2024, baada ya kuanguka kutoka kwenye orofa ya tatu ya hoteli huko Buenos Aires, Argentina.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liam Payne kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |