Letsrecycle.com

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Letsrecycle.com ni tovuti ya Kiingereza ya kuwasilisha habari na taarifa zihusihano na usimamizi wa taka na viwanda vya kuchakata taka. Tovuti hutoa habari na taarifa kila siku na pia ni miongoni mwa wadau wakubwa wa kutoa taarifa ya taka nchini Uingereza. Pia hutaja bei mbalimbali ya taka zilizochakatwa zikiwemo karatasi, vyuma chakavu, plastiki, vioo na mbao. Ni maalumu tu kwa ajili ya wananchi na biashara za Uingereza, Mamlaka za ndani na vikundi vya kijamii vinavyojihusisha na kuchakata na usimamizi wa taka[1]. Pia tovuti hukubali michango na hadithi za watu mbalimbali

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Recycling and Waste Management News". letsrecycle.com (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2022-05-07.