Leo Fender
Clarence Leonidas Fender (anajulikana pia kama Leo Fender; Agosti 10, 1909 - Machi 21, 1991) alikuwa mtengenezaji wa ala za muziki wa Amerika.
Alianzisha kampuni inayoitwa Fender Electric Instrument Manufacturing Company. Inafanya gitaa za umeme, gita za besi za umeme, na amplifaya za gitaa. Leo Fender alitengeneza gitaa za umeme ambazo aliziita Telecaster na Stratocaster. Fender pia alitengeneza gitaa ya besi ya kwanza, ambayo aliiita Precision Bass. Mnamo miaka ya 1960, Fender alitengeneza gitaa nyingine ya besi, ambayo aliiita Jazz Bass.
Ala hizo zote (Telecaster, Stratocaster, Precision Bass, na Jazz Bass) zilikuwa maarufu. Kampuni ya Fender iliuza maelfu na maelfu ya vyombo hivi. Bendi nyingi za muziki wa rock na pop kutoka miaka ya 1960 hadi 2000 zimetumia gitaa hizo za umeme.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- media kuhusu Leo Fender pa Wikimedia Commons
- Fender Musical Instruments website
- G&L Guitars website
- Phyllis Fender Interview – NAMM Oral History Library (2003)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leo Fender kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |