Lech Wałęsa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lech Walesa (2009)

Lech Walesa (Kipoland: Lech Wałęsa (inatamkwa [lɛx vaˈwɛ̃sa]) (amezaliwa tar. 29 Septemba 1943) alikuwa mfanbyakazi wa mameli na mwanasiasa ambaye amezoeleka kuwa kama kiongozi wa Solidarity na Rais wa zamani wa Poland. Mwaka wa 1983, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobeli ya Amani.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Wałęsa alizaliwa mjini Popowo, Poland, mnamo tar. 29 Septemba ya mwaka wa 1943, kwa baba seremala na mkewe. Alihitimu elimu ya msingi na baadaye shule ya ufundi, kabla ya kuingia Lenin Shipyard (kampuni la ujenzi wa mameli) huko mjini Gdańsk (Stocznia Gdańska im. Lenina, sasa hivi Stocznia Gdańska) akiwa kama fundi wa masuala ya umeme mnamo mwaka wa 1970. Kunako mwaka wa 1969 amemwoa Bi. Danuta Gołoś, na wawili hao sasa hivi wana watoto wanane. Mtoto wake wa kiume anaitwa Jarosław Wałęsa ni Mbunge katika bunge la Poland. Lech Wałęsa ni mt'iifu wa Kanisa Katoliki, na akasema kwamba imani yake imemsaidia daima akiwa na shida wakati wa harakati za Solidarity.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lech Wałęsa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.