Le Canadien

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Le Canadien
Ukurasa wa kwanza wa toleo la kwanza la Le Canadien mnamo 22 Novemba 1806
Jina la gazeti Le Canadien
Aina ya gazeti *. Gazeti la lugha ya Kifaransa
*. Gazeti la kila wiki
Lilianzishwa 22 Novemba 1806
Eneo la kuchapishwa Lower Kanada
Nchi Kanada
Mwanzilishi Pierre-Stanislas Bédard
Mmiliki Joseph-Israël Tarte
Mmiliki wa mwisho
Makao Makuu ya kampuni Quebec City, Montreal
Lilikwisha 11 Februari 1893
Likaanzishwa tena katika mwaka wa 2007

Le Canadien lilikuwa gazeti katika lugha ya Kifaransa lililochapishwa katika eneo la Lower Kanada tangu 22 Novemba 1806 hadi 14 Machi 1810. Kaulimbiu yake ilikuwa :"Nos institutions, notre langue et nos droits"( Taasisi zetu, lugha yetu, haki zetu). Lilichapishwa kila Jumamosi na malipo ya kuagiza matoleo ya mwaka mzima yalikuwa shilingi kumi/ chelin kumi. Le Canadien lilianzishwa tena katika mwaka wa 2007 kama gazeti la kitaifa la maendeleo ya kijamii na si la faida, na ,pia, kama la wasomaji wa kimataifa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Gazeti hili lilianzishwa katika jiji la Quebec City na mwanasheria Pierre-Stanislas Bédard na wenzake: François Blanchet, Jean-Antoine Panet, Jean-Thomas Taschereau na Joseph Le Vasseur Borgia Wakati huo, hao wote walikuwa wabunge katika Bunge la Lower Kanada. Mhariri alikuwa Jean-Antoine Bouthillier. Gazeti hili likakua haraka hadi likawa sauti ya Parti canadien (chama cha Kanada) katika vita yao dhidi ya chama cha Uingereza na serikali ya Gavana James Craig.

Tarehe 17 Machi 1810, vyombo vya habari na majarida ya ofisi za uhariri za rue Saint-François yakashikwa na serikali. Mchapishaji Charles Lefrançois akafungwa jela na askari wakaanza kuwatafuta wapinzani wengine jijini. Gazeti la Quebec Mercury ,hapo awali, lilikuwa limesema kuwa Wafaransa wa Kanada na Waamerika walikuwa wakipangia Uingereza njama. Siku mbili baadaye, hakuna watu waliokuwa wakipanga njama waliokuwa wamepatikana. Waanzilishi Bédard, Blanchet na Taschereau walikamatwa, baadaye, na pia kufungwa jela.

Wafungwa hawa walikataa habeas corpus.Walipokuwa gerezani, Bédard akachaguliwa kuwa mgombea wa bunge katika eneo la Surrey na akachaguliwa na raia katika uchaguzi wa 27 Machi 1810. Katika mwaka wa 1811, Mbunge Louis-Joseph Papineau alimwomba Gavana Craig kufuta mashtaka yote ya Bédard lakini gavana alikataa. Bédard ,hatimaye, aliachiliwa kutoka gereza ,Bunge lilipofungwa. Hakupelekwa korti hata siku moja.

Gazeti hilo lilichapishwa tena mara chache. Hatimaye, Le Canadien liliacha kuchapishwa mnamo 11 Februari 1893 likimilikiwa na Joseph-Israël Tarte.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ The Canadian "About us"
  2. ^ "Le Canadien". Towards Confederation. Library and Archives Canada.
  3. ^ Provost, Honorius (1987). "Jean-Thomas Taschereau". Dictionary of Canadian Biography Online.
  4. ^ Brassard, Michèle; Hamelin, Jean (1994). "Joseph-Israël Tarte". Dictionary of Canadian Biography Online.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]