Lango:Tanzania/Makala nzuri/1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dar es Salaam

Dar es Salaam (Kiarabu دار السلام [tafsiri: "Nyumba ya Amani"] Dār as-Salām, cf. "Yer u-salem"), zamani iliitwa Mzizima, ni jiji kubwa nchini Tanzania. Lenye wakazi wapatao 2,500,000, na pia ndiyo mji tajiri nchini na kituo kitovu kikubwa cha uchumi wa Tanzania. Ingawa jiji la Dar es Salaam lilipoteza hadhi yake ya kuwa mji mkuu mnamo mwaka wa 1966 badala yake mji mkuu ukawa Dodoma. Lakini ofisi ya rais na wizara nyingi bado zinafanya kazi Dar es Salaam ambayo hali halisi ni makao makuu ya serikali. (Soma zaidi...)