Lango:Kenya/Makala nzuri/1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nairobi

Nairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mmojawapo wa mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Afrika. Kulingana na sensa ya 2009, Nairobi ina wakaaji 3,138,295. Pamoja na vitongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Afrika.

Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkare nairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi." Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng. (Soma zaidi...)