Kuruka kwa upondo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamume anaruka juu.

Kuruka kwa upondo (kwa Kiingereza: Pole vault[1]) ni riadha ambayo mtu anatumia upondo (fimbo) mrefu kuruka juu. Mchezo wa Kuruka kwa upondo ulianzia katika Ugiriki wa kale. Ni tukio katika michezo ya olimpiki kwa wanaume tangu miaka ya 1896 na kwa wanawake tangu miaka ya 2000.

Kuruka kwa upondo kuna misimu miwili. Msimu wa kwanza huwa katika majira ya joto na wanariadha wanashindana ndani. Msimu wa pili huwa katika majira ya kuchipua na wanariadha wanashindana nje. Wanaume na wanawake wanashindana tofauti. Rekodi ya ulimwengu kwa wanaume ni mita 6.16 (20ft 2.5in) na Renaud Lavillenie kutoka Ufaransa. Kwa wanawake ni mita 5.06 (16ft 7in) na Telena Isinbayeva kutoka Urusi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Miaka mingi iliyopita, watu walitumia fimbo kuvuka maeneo magumu ya asili katika Netherlands. Mashindano ya pole vault usawa bado kutokea huko.

Ushindani wa kuruka kwa upondo wa kwanza ulikuwa katika London Gymnastics Society katika Uingereza. Ushindani wa kwanza katika Olympiki ulikuwa mwaka 1896.

Teknolojia katika kuruka kwa upondo ilibadalika sana. Awali, wanariadha walitumia upondo wa chuma na waliruka ndani mchanga. Wanariadha hawakuikunja upondo. Kwa miaka mingi, mwanariadha wameanza kutumia upondo wa “carbon fiber” au “fiberglass”. Sasa, mwanariahda wanaiinamisha sana upondo kuruka juu. Upondo wa “carbon fiber” au “fiberglass” unapinda kuwezesha watu huruka juu sana.

[1]Johannes Stromhaug anaruka juu katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania State. Picha na S. Oravec

Bao[hariri | hariri chanzo]

Michezo ya kuruka juu (high jump[2]) na kuruka kwa upondo ni michezo inayofanana, kwa hiyo alama za ushindi hufanana pia. Kwa sababu kuruka juu (high jump) na kuruka kwa upondo ni michezo inayofanana, hupata alama kama sawa. Wanariadha wanaweza kuchagua kuingia ushindani katika urefu wowote. Mwanariadha ana majaribu matatu kuruka urefu. Kama mwanariadha anaruka juu, ana ana nafasi tatu za kujaribu matatu katika urefu unaofuata. Urefu unaongozeka mpaka anabaki mwanariadha mmoja. Mwanariadha huondelewa wakati anaposhindwa katika nafasi za majaribio matatu mfululizo. Wakati wanariadha wanapopata alama sawa, wanajaribu urefu tena. Wanadriadha wote wanaposhindwa kuruka urefu fulani, urefu hupunguzwa. Wanariadha wanapofanikiwa urefu fulani, urefu huongezwa. Hii huendelea mpaka mwanariadha mmoja anafanikiwa na mwingine anashindwa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Pole vault", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-11-27, iliwekwa mnamo 2019-12-04
  2. "High jump", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-11-22, iliwekwa mnamo 2019-12-05
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kuruka kwa upondo kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.