Kupanuka kwa kucha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Clubbing
Clubbing.svg
Clubbing of the fingernail. The red line shows the outline of a clubbed nail.
ICD-10R68.3
ICD-9781.5
Upanuziviungo

Kupanuka kwa kucha [1] (ambao pia unajulikana kama "vidole vya kiweo cha kuku," "vidole vya Hippocrates," na "Vidole vya kioo cha saa" [1] ) ni ulemavu wa vidole na kucha inayohusishwa na magonjwa kadhaa, hasa ya moyo na mapafu. [2] :656 Hippocrates huenda ndiye alikuwa wa kwanza kurekodi habari kuhusu upanuzi kama ishara ya ugonjwa, na hivyo tukio hilo mara kwa mara huitwa vidole vya Hippocrates.

Upanuziviungo wenye asili isiyojulikana unaweza pia kutokea na katika 60% ya matukio hakuna ugonjwa wa kimsingi unaohusishwa nao. [3]

Ishara na dalili[hariri | hariri chanzo]

Upanuzi hukua katika hatua tano: [4]

 1. Kubadilikabadilika na kulainika kwa msingi wa kucha (kusongasonga zaidi)
 2. Kupotea kwa pembe ya kawaida iliyo chini ya 165° (pembe ya Lovibond) kati ya msingi wa kucha na ngozirundo la ukucha(kutikula)
 3. Kukunjika zaidi kwa ngozirundo la ukucha
 4. Kunenepa kwa distali yote (sehemu ya mwisho) wa kidole (unaofanana na kiweo cha kuku)
 5. Kumetameta na hali ya kuwa na mistari kwenye ukucha na ngozi

Uchunguzi wa Schamroth au uchunguzi wa dirisha wa Schamroth (ambao awali ulifanywa na mtaalamu wa moyo kutoka Afrika Kusini Dkt Leo Schamroth kwa mwili wake mwenyewe [5] ) ni uchunguzi maarufu wa upanuziviungo. Wakati ambapo distali ya mifupa inayounda vidole (iliyo karibu zaidi na ncha ya vidole) katika vidole vinavyolingana vya mikono ya pande zilizoelekeana kinyume zinawekwa moja kwa moja upande kwa upande (weka kucha za mikono tofauti za kidole kilekile upande kwa upande, ukucha kwa ukucha), "dirisha" ndogo lenye umbo la almasi kwa kawaida huonekana kati ya misingi ya kucha. Ikiwa dirisha hili halionekani, upimaji huo ni chanya na upanuziviungo upo.

Uaguzi[hariri | hariri chanzo]

Wakati upanuziviungo unapotambuliwa katika wagonjwa, madaktari watajaribu kubaini chanzo chake. Kwa kawaida, wao hutekeleza jambo hili kwa kupata historia ya hali ya afya-umakini huwekwa hasa kwa kuchunguza mapafu, moyo, na matatizo yanayohusiana na utumbo- na kufanya uchunguzi wa kimatibabu, ambao unaweza kufichua vipengele husika vinavyohusika na uaguzi. Uchunguzi wa ziada kama vile eksirei ya kifua na Uchunguzipicha kifuani pia unaweza kufanywa. [4]

Mahusiano ya ugonjwa[hariri | hariri chanzo]

Ingawa magonjwa mengi yanayohusishwa na upanuziviungo (hasa magonjwa ya mapafu), taarifa hizi bado hazijadhibitishwa kwa kiwango fulani. Uchunguzi unaotazamiwa wa wagonjwa wenye upanuziviungo bado haujafanywa, na hivyo hakuna ushahidi kamili kuhusu mahusiano hayo.

Upanuziviungo uliotengwa[hariri | hariri chanzo]

Upanuziviungo katika vidole ya mwanamke mwenye umri wa miaka 33 anayeugua ugonjwa wa Eisenmenger.

Upanuziviungo unahusishwa na:

 • Ugonjwa wa mapafu:
  • Saratani ya mapafu, hasa seli kubwa (35% ya kesi zote), isiyoonekana sana katika kansa ya mapafu ya seli ndogo[6]
  • Ugonjwa wa mapafu unaoathiri tishu na mifuko ya hewa
  • Kifua kikuu
  • Magonjwa ya mapafu yanayomfanya mtu atoe usaha: nekrosi ya tishu ya mapafu, utungaji usaha, uvumbe koromeo, uvimbe wa nyuzi
  • Mesothelioma
  • Muunganisho au mwanya usio wa kawaida kati ya ateri na vena
 • Ugonjwa wa moyo:
  • Ugonjwa wowote unaoshirikisha haipoksia sugu
  • Ugonjwa wa moyo unaotokana na ukosefu wa oksijeni ya kutosha kwenye damu katika watoto waliozaliwa (sababu kuu magonjwa ya moyo)
  • Maambukizi ya bakteria katika valvu za moyo kwa kiwango kati ya kali na sugu
  • Miksoma ya ateri (kivimbe hafifu)
 • Ya utumbo na ini, kichirizi nyongo, kibofu nyongo:
  • Ufyonzaji mbaya
  • Ugonjwa wa Crohn na vidonda vya kolitisi
  • Sirosisi, hasa katika homaini ya msingi inayosababishwa na nyongo [7]
  • Ugonjwa wa upungufu wa hewa, tatizo la sairosisi[8]
  • Matumizi mabaya ya madawa ya kuharisha
  • Poliposisi
  • Saratani ya umio
 • Mengine:
  • Utoaji wa kiwango cha juu cha homoni za kikoromeo (akropachia ya tezi) [9]
  • Upanuziviungo wa kifamilia na kimbari na clubbing rangi na "awamu ya kwanza ya upanuziviung" (watu wenye asili ya Afrika mara nyingi huwa na kile kinachoonekana kuwa upanuziviungo)
  • Kasoro zinazohusiana na mishipa ya damu katika mkono ulioathirika kama vile aneurisimi ya ateri kwapa (upanuziviungo wa upande mmoja)
  • Thaimoma
  • Thalasemia

HPOA (Haipatrofiki ya osteoathropathia ya mapafu)[hariri | hariri chanzo]

Ukaguzi wa mifupa ya mgonjwa mwenye HPOA

Aina maalum ya upanuziviungo ni haipatrofiki ya osteoathropathia ya mapafu, inayojulikana barani Ulaya kama Ugonjwa wa Pierre Marie-Bamberger. (Katika mbwa hali hii hujulikana kama osteoathropathia ya haipatrofiki.) Huu ni mchanganyiko wa upanuziviungo na kupanuka kwa peristiamu (tishu unganifu ya mifupa) na utando wa sinovia (bitana ya viungo), na mara nyingi hutambuliwa kama ugonjwa wa baridi yabisi katika kipindi cha awali. Mara nyingi ugonjwa huu huhusishwa na kansa ya mapafu.

HOA (Haipatrofiki ya osteoathropathia) ya msingi[hariri | hariri chanzo]

Haipatrofiki ya osteoathropathia ya msingi ni HPOA isiyo na dalili za ugonjwa wa mapafu. Aina hii ina kipengele cha kurithiwa, ingawa hali ya moyo isiyo ya kawaida na iliyo ngumu kutambua huweza kupatikana mara kwa mara. Inajulikana kama ugonjwa wa Touraine-Solente-Golé, ambalo lilikuwa ni jina la mtu. Hali hii imehusishwa na kubadilika kwa ishara ya jeni ya kromosomu ya nne (4q33-q34) kwa kimeng'enya 15-haidroksiprostaglandini ya dihaidrojenesi (HPGD); hii husababisha kuvunjika kwa prostaglandini E2 na kiwango cha juu cha dutu hii. [10]

Pathofisiolojia[hariri | hariri chanzo]

Chanzo kamili cha upanuziviungo wa mara kwa mara haijulikani, na kuna nadharia nyingi zinazojaribu kueleza chanzo chake. Upanukaji wa mishipa ya damu (mishipa ya damu iliyofura), utoaji wa ugiligili wa kisababishi cha ukuaji (kama vile kisababishi cha ukuaji kinachotokana na chembe za kugandisha damu na kisababishi cha ukuaji kinachotokana na hepatositi) kutoka kwenye mapafu, na taratibu zingine zimependekezwa. Kutambuliwa kwa magonjwa katika metaboli ya prostaglandini katika osteoathropathia ya msingi kumesababisha kutolewa kwa mapendekezo kuwa uzalishaji wa kupindukia wa PGE2 na tishu nyingine unaweza kuwa ndio chanzo cha upanuziviungo. [10]

Epidemolojia[hariri | hariri chanzo]

Marudio halisi ya upanuziviungo kati ya watu haijulikani. Utafiti wa 2008 ulitambua upanuziviungo kwa 1% ya wagonjwa wote waliolazwa katika idara ya tawi la tiba linaloshughulikia dawa zitumiwazo kutibu magonjwa yasiyohitaji upasuaji. Kati ya hizo, 40% walitambuliwa kuwa na kiwango kikubwa cha ugonjwa ya msingi unaotokana na sababu mbalimbali, huku 60% walikuwa hawana matatizo yoyote ya kiafya baada ya uchunguzi wa kina na waliendelea kuwa na afya nzuri katika mwaka uliofuata. [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 Rapini, Ronald P.; Bolognia, Jean L.; Jorizzo, Joseph L. (2007). Dermatology: 2-Volume Set. St. Louis: Mosby. ISBN 1-4160-2999-0. 
 2. Freedberg, et al. (2003). Fitzpatrick's Dermatology in General Medicine. (6th ed.). McGraw-Hill. ISBN 0071380760.
 3. 3.0 3.1 Vandemergel X, Renneboog B (Julai 2008). "Prevalence, aetiologies and significance of clubbing in a department of general internal medicine". Eur. J. Intern. Med. 19 (5): 325–9. doi:10.1016/j.ejim.2007.05.015 . PMID 18549933 .
 4. 4.0 4.1 Myers KA, Farquhar DR (2001). "The rational clinical examination: does this patient have clubbing?". JAMA 286: 341–7. doi:10.1001/jama.286.3.341 . PMID 11466101 .
 5. Schamroth L (Februari 1976). "Personal experience". S. Afr. Med. J. 50 (9): 297–300. PMID 1265563 .
 6. Sridhar KS, Lobo CF, Altman RD (1998). "Digital clubbing and lung cancer" (PDF). Chest 114: 1535–37. doi:10.1378/chest.114.6.1535 . PMID 9872183 . http://www.chestjournal.org/cgi/reprint/114/6/1535. Retrieved 2010-11-30.
 7. Epstein O, Dick R, Sherlock S (1981). "Prospective study of periostitis and finger clubbing in primary biliary cirrhosis and other forms of chronic liver disease". Gut 22 (3): 203–6. doi:10.1136/gut.22.3.203 . PMID 7227854 .
 8. Naeije R. Hepatopulmonary portopulmonary syndrome na shinikizo la damu. Med Uswisi Wkly. 2003; 133:163-9. PMID 12,715,285.
 9. -724565997 at GPnotebook
 10. 10.0 10.1 Uppal S, Diggle CP, Carr IM, et al. (Juni 2008). "Mutations in 15-hydroxyprostaglandin dehydrogenase cause primary hypertrophic osteoarthropathy". Nat. Genet. 40 (6): 789–93. doi:10.1038/ng.153 . PMID 18500342 .