Nenda kwa yaliyomo

Kuoza kwa meno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuoza kwa meno
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyUganga wa meno Edit this on Wikidata
ICD-10K02.
ICD-9521.0
DiseasesDB29357
MedlinePlus001055

Kuoza kwa meno (caries ni neno la Kilatini kutoka "rottenness"[1]), pia hujulikana kama kuoza kwa jino, kaviti, au caries, ni kuharibika kwa meno kutokana na shughuli za bakteria.[2] Kaviti inaweza kuwa na aina tofauti za rangi kutoka kijani kibichi hadi nyeusi.[3] Dalili zinaweza kujumuisha maumivu na ugumu wa kula chakula.[4][3] Matatizo yanaweza kujumuisha inflamesheni ya tishu zinazozunguka jino, kupoteza jino, na maambukizi au usaha hutokea.[1][3]

Kisababishi[hariri | hariri chanzo]

Bakteria huharibu tishu ngumu ya meno (enameli, dentini na sementamu) kwa kutengeneza asidi kutoka kwa mabaki ya chakula kwa sehemu ya jino.[5] Sukari nyepesikatika chakula ni chanzo cha nguvu ya kimsingi ya bakteria na kwa hivyo lishe ya juu iliyo na sukari nyepesi ni swala la hatari.[5] Ikiwa uharibifu wa madini ni mkubwa kuliko ujenzi kutoka kwa vyanzo kama vile mate, matokeo ni kuoza kwa meno.[5] Maswala ya hatari inajumuisha hali zinazoleta matokeo ya mate kidogo kama vile: ugonjwa wa kisukari, Sindromu ya sjogren na baadhi ya matibabu.[5] Matibabu yanayopunguza utoaji wa mate yanajumuisha antihistamines na dawa za kupunguza makali na mengine.[5] Kuoza kwa meno pia kunahusishwa na umasikini usafishaji wa mdomo, na kurudi hali ya hapo awali ufizi wa meno inayoleta athari kwa mizizi ya meno.[6][2]

Uzuiaji na matibabu[hariri | hariri chanzo]

Uzuiaji hujumuisha: usafishaji wa meno kila wakati, lishe iliyo na sukari ya chini na kiwango kidogo cha floridi.[5][4] Kupiga meno mswaki mara mbili kwa siku na kusafisha katikati ya meno mara moja kwa siku unapendekezwa na wengi.[2][7] Floridi inaweza kutokana na maji, chumvi au dawa ya meno na vyanzo vinginevyo.[4] Kutibu meno ya mama yaliyooza kunaweza kupunguza hatari kwa watoto wake kwa kupunguza idadi fulani ya bakteria.[5] Uchunguzi unaweza kuleta utambuzi wa mapema.[2] Kulingana na kiwango cha uharibifu, matibabu kadhaa yanaweza kutumika urejeshaji meno kwa hali yake ya kufanya kazi au jino linaweza kutolewa.[2] Hakuna mbinu inayojulikana kurudia hali ya awali viwango vikubwa vya jino.[8] Matibabu yaliyopo katika nchi zinazostawi ni duni kila mara.[4] Paracetamol (acetaminophen) au ibuprofen inaweza kutumiwa kutuliza maumivu.[2]

Epidemiologia[hariri | hariri chanzo]

Kote duniani, takribani watu bilioni 2.43 (asilimia 36 ya idadi ya watu)  wana meno yaliyooza ya kudumu.[9] Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa karibu watu wote wazima huwa na meno yaliyooza kwa wakati fulani.[4] Meno ya watoto wachanga huathiri karibu watu milioni 620 au asilimia 9 ya idadi ya watu.[9] Uozaji wa meno hutokea sana kwa watu wazima na watoto kwa miaka ya hivi karibuni.[10] Ugonjwa huu unapatikana sana katika nchi zinazostawi na kiasi kwa nchi zilizostawi kwa sababu ya matumizi ya sukari kiasi.[2]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Taber's cyclopedic medical dictionary (toleo la Ed. 22, illustrated in full color). Philadelphia: F.A. Davis Co. 2013. uk. 401. ISBN 9780803639096.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 Silk, H (Machi 2014). "Diseases of the mouth". Primary care. 41 (1): 75–90. PMID 24439882.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 Laudenbach, JM; Simon, Z (Novemba 2014). "Common Dental and Periodontal Diseases: Evaluation and Management". The Medical clinics of North America. 98 (6): 1239–1260. PMID 25443675.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 "Oral health Fact sheet N°318". who.int. Aprili 2012. Iliwekwa mnamo 10 Desemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 5.6 SECTION ON ORAL, HEALTH; SECTION ON ORAL, HEALTH (Desemba 2014). "Maintaining and improving the oral health of young children". Pediatrics. 134 (6): 1224–9. PMID 25422016.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Schwendicke, F; Dörfer, CE; Schlattmann, P; Page, LF; Thomson, WM; Paris, S (Januari 2015). "Socioeconomic Inequality and Caries: A Systematic Review and Meta-Analysis". Journal of dental research. 94 (1): 10–18. PMID 25394849.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. SECTION ON ORAL, HEALTH; SECTION ON ORAL, HEALTH (Desemba 2014). "Maintaining and improving the oral health of young children". Pediatrics. 134 (6): 1224–9. PMID 25422016.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Otsu, K; Kumakami-Sakano, M; Fujiwara, N; Kikuchi, K; Keller, L; Lesot, H; Harada, H (2014). "Stem cell sources for tooth regeneration: current status and future prospects". Frontiers in physiology. 5: 36. PMID 24550845.
  9. 9.0 9.1 Vos, T (Des 15, 2012). "Years lived with disability (YLDs) for 1160 sequelae of 289 diseases and injuries 1990-2010: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2010". Lancet. 380 (9859): 2163–96. doi:10.1016/S0140-6736(12)61729-2. PMID 23245607.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Bagramian, RA; Garcia-Godoy, F; Volpe, AR (Februari 2009). "The global increase in dental caries. A pending public health crisis". American journal of dentistry. 22 (1): 3–8. PMID 19281105.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)