Kundi la galaksi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kundi la galaksi HCG 16, ilivyoonekana kwa darubini ya Hubble

Kundi la galaksi (kwa Kiingereza: galaxy group) ni idadi ya galaksi zinazoshikamana katika anga-nje. Maana zinaathiriana kwa njia ya graviti yake. Katika mpangilio huo ni hadi galaksi 50 zinazotazamwa kuwa kundi.

Kama idadi ya galaksi zinazoshikamana ni kubwa zaidi jumla yake ni fundo la galaksi.

Galaksi za kundi moja zinaenea katika nafasi yenye kipenyo cha takriban miakanuru milioni 10 hivi; masi ya galaksi zote kwa pamoja ndani ya kundi ni hadi masi za Jua 1013.[1]

Galaksi yetu ya Njia Nyeupe ni sehemu ya kundi janibu la galaksi pamoja na galaksi 40 hivi nyingine.[2] Pamoja na Njia Nyeupe kuna Galaksi ya Andromeda (inaitwa pia M31) katika kundinyota Mara, ya M33 katika Pembetatu na galaksi ndogo kama Mawingu ya Magellan.

Marejeo

  1. UTK Physics Dept. Groups of Galaxies. University of Tennessee, Knoville. Iliwekwa mnamo September 27, 2012.
  2. Mike Irwin. The Local Group. Iliwekwa mnamo 2009-11-07.
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kundi la galaksi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano