Kituo cha sanaa cha Pakare Paye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kituo cha sanaa cha Pakare Paye (Pakare Paye Arts Centre) ni mojawapo ya mipango ya marehemu mwanamuziki nguli wa Zimbabwe Oliver Mtukudzi [1] [2] [3] ambaye pia alijulikana kama Tuku. [4] [5] [6]

Kituo hicho cha sanaa kilifunguliwa mwaka wa 2004 tarehe 3 Oktoba na kinapatikana mji wa Norton ambao uko umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu wa Harare. Mahali hapo hapo awali palitumika kama ghala.

Sifa kuu ya kituo ni pamoja na Kituo cha Mikutano cha Sam Mtukudzi kilichopewa jina la mtoto wake marehemu Sam (aliyefariki mwaka 2011 kwa ajali ya gari). Kuna mikahawa, nyumba za kulala wageni, ofisi, na pia jukwaa la wazi ambalo linaweza kuchukua watu 3,000. Ukumbi kuu ni viti 200. [7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Tuku leaving Pakare Paye for the last time". 26 January 2019. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-07. Iliwekwa mnamo 2022-03-19.  Check date values in: |date= (help)
  2. "Tribute to an icon". 27 January 2019.  Check date values in: |date= (help)
  3. Chronicle, The. "Farewell humble giant". The Chronicle. 
  4. newsday (31 October 2011). "Tuku, a serious business person".  Check date values in: |date= (help)
  5. "Tuku unveils free Sunday show at Pakare Paye". 5 March 2018.  Check date values in: |date= (help)
  6. H-Metro. "Pakare Paye’s Valentine’s gig without Tuku". H-Metro. 
  7. Mail, The Sunday. "‘Dzvamu Tsvamu’ at Pakare Paye". The Sunday Mail.