Nenda kwa yaliyomo

Kituo cha Matibabu cha Bugando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kituo cha Matibabu cha Bugando (kwa Kiingereza: Bugando Medical Centre ni kituo cha matibabu cha juu kinachomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Hospitali hiyo inaendeshwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania.

Ni hospitali iliyojengwa na Kanisa Katoliki kati ya mwaka 1968 na 1977. Ilifunguliwa rasmi tarehe 3 Novemba 1971, na Rais mwanzilishi wa Tanzania, Julius Nyerere.

Mnamo mwaka 1972 hospitali ilitaifishwa na serikali. Walakini, miaka 13 baadaye, ilikabidhiwa tena kwa Kanisa Katoliki Tanzania, kwa uelewa kwamba hospitali hiyo inaendeshwa kama hospitali ya rufaa ya Kanda ya Ziwa, ikichukua mikoa 8 kati ya mikoa 31 ya Tanzania (jumla ya watu milioni 14 mwaka 2017), na ushirikiano wa Serikali ya Tanzania.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]