Kitimaguru
Kitimaguru (pia kiti cha magurudumu, kitimagurudumu, kwa Kiingereza: wheelchair) ni kifaa kilichotengenezwa kikiwa na kiti pamoja na magurudumu kwa madhumuni ya kumsaidia majeruhi, wagonjwa wasio na nguvu ya kutembea au watu wenye ulemavu kukalia na kujisukuma, kusukumwa na mtu mwingine au kujiendesha kwa mashine za otomatiki kwa lengo la kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kiti hicho huwa kimeundwa hivi kwamba mgonjwa atapata starehe ya kuketi.
Kitimaguru kinaweza kusukumwa na mtu aliyekikalia au na mwingine anayemhudumia.
Huenda pia kikawa na vidhibiti ili anayebebwa aweze kudhibiti mwendo wa kigari kile.
Kitimaguru hupatikana pia kwa wenye ulemavu wanaoshindana katika uga wa spoti.