Kiteso
Kiteso (pia inajulikana kama Iteso au Ateso) ni lugha ya Kinilo-Sahara, inayozungumzwa na kabila ya Wateso nchini Uganda na Kenya. Ni mmojawapo wa nguzo ya lugha za Kiteso-Kiturkana.
Katika sensa ya watu ya mwaka wa 1991 idadi ya watu karibu 999,537 ilikuwa inazungumza lugha ya Kiteso kote nchini Uganda. Watu ambao idadi yao iliwastaniwa kuwa laki 279 nchini Kenya pia waliizungumza lugha hii. Kodi yake ya SIL ni TEO.[1]
Asili ya Lugha ya Kiteso ni eneo linaloitwa Teso.
Lugha ya kawaida
[hariri | hariri chanzo]Habari --- yoga
U hali gani? --- Ijai biai (umoja)
Ijaasi biai (wingi)
Salama salmini, na wewe je? Ejokuna, arai ijo?
Njema --- ejokuna
Waitwaje? ---
Ingai bo ekon'kiror?
Jina langu ni ... ---
Eka'kiror ...
Jina ---
Ekiror
Ni vizuri kukujua. ---
Eyalama ewanyun (pia: Eyalama aanyun)
Tutaonana baadaye tena ---
Awanyunos Bobo
Kitabu --- Eitabo
Sababu --- Naarai
Sentensi ya kwanza katika Biblia inaweza kutafsiriwa kama Ageunet, abu Edeke Kosub akwap had akuju (kwa Kiswahili: "Mwanzoni Mungu aliumba dunia na mbingu").
Jinsia
[hariri | hariri chanzo]Kama lugha zingine nyingi, Kiteso pia ina majina ya jinsia. Katika maneno ya lugha ya Kiteso, jinsia huashiriwa kwa kawaida katika herufi ya kwanza ya neno. Ikiwa herufi E au herufi O ni herufi ya kwanza katika jina basi jina hilo ni la kiume. Ikiwa herufi A ni herufi ya kwanza katika jina basi jina hilo ni la
Mwanaume wa Kiteso anaweza kujiita Etesot na mwanamke anaweza kujiita Atesot
Jimbi au jogoo ukipenda anajulikana kwa lugha ya Kiteso kama "Ekokor " na kuku anajulikana kama "Akokor ".
Kama lugha zingine ambazo zina majina ya kijinsia, mambo ambayo kwa kawaida hayawezi kuwekwa katika jamii ya kijinsia bado yanaweza kuwekwa kwa jamii kimakusudi. Mfano moja wa mambo au maneno haya ni "Etogo " ambayo inamaanisha nyumba kwa lugha ya Kiteso na hospitali inaitwa "Adekis ". Shati inajulikana kama "Esaati ".
Neno "Akwii " linamaanisha majani, hata hivyo kulitamka neno hilo kwa msongo uliorefushwa mwishoni kunaibadilisha neno hilo kuwa jina la mwanamke. Kubadilisha jina hilo kuwa "Okwii " hubadilisha neno hilo kuwa jina la mwanaume.
Idadi
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa kuhesabu katika lugha ya Kiteso, idadi ya 6 hutafsiriwa kama 5 +1, 7 ni 5 +2 na kadhalika. Katika mtindo huo 16 ni 10 +5 +1, 17 ni 10 +5 +2. 21 tena ni 20 +1, 26 pia ni 20 +5 +1. Hakuna neno katika lugha ya Kiteso inayoashiria idadi kubwa isiyojulikana. Neno sufuri ni Enooti .
- Idiopet au Ipe
- Iyarei
- Iuni
- Iwongon
- Ikanyi
- Ikanyikadiop au Ikanyikape
- Ikanyikaare
- Ikanyilauni
- Ikanyikawongon
- Itomon
- Itomonkadiop au Itomonkape
- Itomonkaarei
- Itomonkauni
- Itomonkawongon
- Itomonkakany
- Itomonkakanyikaape
- Itomonkakanyikaarei
- Itomonkakanyikauni
- Itomonkakanyikawongon
- Akaisaarei
- Akaisaareikayediopet
- Akaisaareikakanuyarei
- Akaisaareikakanuiuni
Idadi kubwa ni kama ifuatavyo: --
Idadi | idadi ya Kiteso katika maneno | |
---|---|---|
[45] | Akaisauni | |
40 | Akaisaagon | |
50 | Akaisakany | |
60 | Akaisakanyikaape | |
60 | Akaisakanyikaape | |
70 | Akaisakanyikaarei | |
80 | Akaisakanyikauni | |
[75] | Akaisakanyikawogon | |
100 | Akwatat | |
101 | Akwatatkidiopet |
| |)
Maneno yaliyokopwa
[hariri | hariri chanzo]Lugha ya Kiteso imekopa idadi ya maneno, kimsingi kutoka Kilatini, ambayo baadaye ilikwenda kutumika katika lugha ya Kiingereza, hivyo basi mfanano.
- Herufi E katika maneno ya Kiteso hutamkwa kama É au "ay".
Maneno yenye alama ya asteriski (*) huonyesha kwamba herufi ya mwisho katika neno hilo la Kiteso ni kimya.
Neno la Kiswahili | Neno la Kiteso | |
---|---|---|
Gari | Emotoka | |
Runinga | Etelevision | |
Radio | Eredio | |
Mashine ya Fax | Afakis mashin | |
Barua Pepe | E-emeilo * | |
Intaneti | E-Intanet | |
Tarakilishi | Akompuita | |
Simu | Etelefoni * | |
Kicheza Rekodi | A rekod puleya | |
Kicheza CD | A Sidi puleya | |
Kicheza DVD | Adividi puleya | |
Diski | Adisiki * | |
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.ethnologue.com/language/teo Accessed 2007/07/09