Nenda kwa yaliyomo

Kisiwa cha Kusini (New Zealand)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kisiwa cha kusini)
Mahali pa New Zealand duniani upande wa kusini mashariki ya Australia
Visiwa vikuu vya New Zealand kwa macho ya satelaiti

Kisiwa cha Kusini ni kimoja cha visiwa viwili vikuu vya New Zealand ilhali ni kisiwa kikubwa zaidi. Mlangobahari wa Cook unakitenganisha na Kisiwa cha Kaskazini.

Eneo lake ni km2 151,215 na idadi ya wakazi ni 1,138,000 ambayo ni robo moja ya wananchi wa New Zealand.

Jina lake la Kimaori ni Te Wai Pounamu .

Mji mkubwa ni Christchurch.