Kisabaki
Mandhari
Kisabaki ni lugha za Kibantu jamii ya Kiswahili zilizopewa jina la Mto Sabaki. Lugha za Kisabaki, mbali ya Kiswahili, zinahusisha Ilwana (Malakote) na Pokomo kwenye Mto Tana nchini Kenya; Mijikenda, inayozungumzwa katika pwani ya Kenya; Kikomoro, katika Visiwa vya Komoro; na Mwani, inayozungumzwa kaskazini mwa Msumbiji[1].
Katika uainishaji wa lugha wa Guthrie, Kiswahili kiko katika eneo la Kibantu G, ambapo lugha nyingine za Kisabaki ziko katika ukanda E70, kwa kawaida chini ya jina Kinyika, kama ifuatavyo:
- Ilwana (Malakote) (E.701)
- Pokomo (E.71)
- Mijikenda (E.72–73) (kasikazini (Nyika), Segeju, Digo, Degere)
- Comorian katika makundi mawili, Magharibi (Shimwali na Shingazidja) na Mashariki (Shimaore na Shindzwani)
- Mwani (Msumbbiji)
- Makwe Swahili (Brava, Somalia), Coastal Swahili (Lamu, Mombasa, Zanzibar), Pemba Swahili (Pemba, Mafia)
Kwa kuongeza, kuna krioli na pijini kadhaa za Kiswahili: Cutchi-Swahili, Kiswahili), Kikeya.Kingereza, Sheng, Shaba kiswahili (Katanga Swahili, Lubumbashi Swahili), Ngwana (Congo kiswahili), Kikeya.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Derek Nurse & Thomas J. Hinnebusch, 1993, Swahili and Sabaki: a linguistic history.